Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka akisoma risala yake kwenye hafla hiyo ambapo alitoa pongezi
kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ya
Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Umoja huo kuhakikisha
malengo ya milenia yanafikiwa kwa asilimia mia moja.
Profesa Tibaijuka na Bw. Rodriguez wakijiandaa kufanya "cheers" ya kuutakia kheri Umoja huo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Tibaijuka
kuzungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez wakigonganisha glass "Cheers" kuutakia kheri Umoja huo
kwa kutimiza miaka 69.
Tanzania
imetaka jumuiya za kimataifa na washirika wa maendeleo kuhakikisha
wanashirikiana na Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba madhumuni ya
kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) yanafikiwa.
Umoja
wa Mataifa ulianzishwa miaka 69 iliyopita kuhakikisha amani, maendeleo
na ukuaji wa demokrasia ili kuifanya dunia hii kuwa mahali bora pa
kuishi.Kauli ya Tanzania imetolewa kupitia Waziri wake wa Ardhi na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka mwishoni mwa wiki wakati wa
kilele cha sherehe za miaka 69 ya Umoja wa Umoja.
Alisema hayo katika hafla ya mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya UN iliyofanyika jijini dar es salaam.
Alisema
jukumu la Umoja wa Mataifa la kuwezesha maisha bora duniani haliwezi
kufanikiwa kama kusipokuwapo ushirikiano wa dhati wa kukomesha
changamoto zinazokabili dunia hii kama umaskini uliokithiri, ugaidi na
magonjwa.
Alisema
kwa miongo mitatu Umoja wa Mataifa umejituma katika kutekeleza wajibu
wake hasa katika kuleta usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira, kuelekeza
maendeleo ya pamoja na kuhakikisha amani inapatikana.
Alisema
mikutano mbalimbali ya kimataifa iliyofanyika kama ile ya Stockholm,
Vancuva, Beijing ililenga kuweka msimamo wa pamoja ambao unawezesha
dunia kuwa mahali pa amani ambapo mataifa yanashirikiana kuiweka salama
dunia, kwa kuangalia changamoto za demokrasia,mabadiliko ya hali ya hewa
na usawa wa binadamu huku suala la wanawake na watoto likitiliwa
maanani.
Alisema
juhudi za Umoja wa Mataifa umewezesha mabadiliko makubwa kuwepo ambapo
dunia kama moja inafanya juhudi za kuimarisha ushiriki wa wanawake
katika maendeleo, kuwa na sauti moja katika kukabiliana na majanga
mbalimbali yakiwemo vita na magonjwa.
Hata
hivyo alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika sekta
mbalimbali za afya, amani na maendeleo na kuleta usawa wa jinsia na
kushughulikia afya na maendeleo ya wanawake na demokrasia, bado UN ina
changamoto kubwa inayoambatana na maendeleo yaliyopo.
Alisema
umaskini uliokithiri na ugaidi umekuwa chanzo kipya cha migogoro
inayotishia amani na maendeleo ya dunia. Alizitaka nchi wanachama
kuungana kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinatokomezwa.
Akimkaribisha
Waziri Tibaijuka kuongea Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez, alisema kwamba wamefurahishwa na hatua
iliyofikiwa na Tanzania katika kutekeleza malengo ya milenia na kwamba
Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha
kwamba malengo yale ambayo hayakufikiwa yanafanyiwa kazi katika mpango
wa maendeleo ujao.
Aidha
alishukuru Tanzania kwa kuipatia UN eneo la kujenga makazi kwa ajili ya
mashirika yake yanayofanyakazi nchini . Pia alisema kwamba wakati Umoja
wa Mataifa unajikita katika kufanikisha maisha bora kwa wakazi wa
duniani, inatambua changamoto zake zilizopo sasa ambapo mamilioni ya
wananchi wanateseka kwa kunyonywa, usafirishaji haramu wa watu na
kufanyishwa utumwa wa kingono.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia)
akiteta jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon
Kochanke wakati wa zoezi la kupokea wageni kwenye hafla mchapalo ya
kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Alisema
ili kuwa na maendeleo na haki ni lengo la Umoja wa Mataifa kuhakikisha
hakuna anayeachwa nyuma katika maendeleo ya kubadili dunia kuwa mahali
bora pa kuishi.
Alisema
wakati mpango wa malengo ya milenia unaisha mwakani ni vyema mataifa
yakaendelea kufikiria kutekeleza yale ambayo haya kuwezekana katika
agenda zao za maendeleo.
Alisema
amefurahishwa na kauli ya serikali ya Tanzania kwamba imejipanga
kuhakikisha inadhibiti ugonjwa wa Ebola na pia kuandaa mipango kwa
vijana kupata ajira na kukabili mabadiliko ya tabia nchi. Aidha katika
hotuba yake amesema kwamba kwa kuzingatia kwamba nguvu kazi kubwa sasa
ni vijana ni vyema jamii ikaacha vijana waongoze kwa kuwa wao ndio
wazazi wa kesho na pia ndio nguvu inayotakiwa katika ubunifu na
uendeshaji wa shughuli za maendeleo.
Aidha
alisema jumuiya ya kimataifa ni lazima itambue ushirikiano kama njia
pekee ya kukabiliana na changamoto za dunia kwani hakuna nchi moja
inayoweza kufanya shughuli yoyote peke yake.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto)
akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka wakati
wa zoezi la kukaribisha wageni kwenye hafla mchapalo ya maadhimisho ya
miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi akiteta jambo na baadhi
ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh.
Lennarth Hjelmaker (waliyeshikana mkono) kwenye hafla mchapalo
iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 69 ya
Umoja huo tangu kuanzishwa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa FAO, Diana Templeman mara baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
Waziri
wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka
akiwasili kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akisherehesha hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi
wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati hafla hiyo ikiendelea.
No comments:
Post a Comment