Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akitoa hotuba yake
wakati wa harambee ya kuchangia ukarabati wa Miundombinu ya Shule ya
Sekondari Enaboishu,kushoto ni Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Masangwa,Mkuu
wa Shule hiyo,Lesion Ole Sekioni na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye ni mhitimu wa Shule
hiyo,Elisante Ole Gabriel.
Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Solomon Maswangwa akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel
aliyebuni mpango wa kuwakutanisha wanafunzi waliosoma Shule hiyo
kuchangia maendeleo ya elimu,yeye akiwa mmoja wao.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi mbalimbali na Wafanyakazi wa Shule ya Enaboishu
Waimbaji wa Empowered Girls Club wakitoa burudani iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
Waimbaji
wa Empowered Girls Club wakifurahia kitita cha Sh.200,000 walizopewa na
mgeni rasmi,Waziri wa Elimu,Dk Shukuru Kawambwa kwa kutoa burudani
iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akipongenzwa na
wanafunzi wa Shule ya hiyo baada ya kufanikisha harambee .
No comments:
Post a Comment