Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia)
akikabidhi funguo za Basi dogo kwa Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
Bwawani, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga(kushoto). Basi
hilo litatumiwa na Wanafunzi katika ziara mbambali za Mafunzo hivyo
kuondoa kero kubwa ya Usafiri shuleni hapo.
Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi
wa Magereza, Emmanuel Lwinga akijaribisha kuwasha gari jipya
lililokabidhiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir
Minja(hayupo pichani) katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne
Bwawani Sekondari yaliyofanyika Oktoba 22, 2014.
Muonekano wa Basi dogo lenye Na. MT. 0341 lililokabidhiwa Oktoba 22,
2014 na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo
pichani) katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari
Bwawani, Mkoani Pwani. Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi wa Bwawani
Sekondari katika ziara mbalimbali za Mafunzo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(aliyevaa
skafu) akiwa meza Kuu amesimama na Viongozi mbalimbali Waalikwa wakati
Wahitimu Wakiimba Wimbo Maalum wa Shule katika Mahafali ya Kumi na Moja
ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari Oktoba 22, 2014(wa pili kushoto)
ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(wa
kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula (wa kwanza kulia) ni Kaimu Mkuu
wa Shule ya Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel
Lwinga.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akikabidhi cheti
kwa Mhitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kidato cha Nne Bwawani
Sekondari Oktoba 22, 2014. Jumla ya Wahitimu 95 wametunukiwa cheti
cha kuhitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule hiyo inayomilikiwa na
Jeshi Magereza, Mkoani Pwani.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja akitoa hotuba
yake fupi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Bwawani
Sekondari yaliyofanyika Oktoba 22, 2014 Mkoani Pwani.
Sehemu ya Wahitimu katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne,
Bwawani Sekondari wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali
wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kikundi cha Wasanii kinachoundwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari
kikijiandaa kutumbuiza mbele ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Kumi na
Moja ya Kidato cha Nne Shule ya Bwawani Sekondari, Mahafali hayo
yamefanyika Oktoba 22, 2014, Mkoani Pwani.
Mama mzazi wa Mhitimu wa Kidato cha Nne kutoka familia ya Kifugaji ya
Kimasai akimbusu mkono Mtoto wake ambaye amehitimu Elimu ya Kidato cha
Nne katika Shule inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, Bwawani Sekondari
iliyopo Mkoani Pwani. Mahafali hayo yamefanyika Oktoba 22, 2014.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa na
Wahitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha
Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza.
Mahafali hayo yamefanyika Oktoba 22, 2014 katika Bwalo la Bwawani
Sekondari, Mkoani Pwani
(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment