Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akifungua rasmi mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia ukuaji wa
uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii
uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini , Alvaro Rodriguez nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya mgeni
rasmi kuwasili kwenye mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia
ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa
jamii uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency,
Kilimanjaro. Picha na Zainul Mzige
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini , Alvaro Rodriguez nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya mgeni
rasmi kuwasili kwenye mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia
ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa
jamii uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency,
Kilimanjaro. Picha zote na Zainul Mzige
Mkurugenzi
wa Programu wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa taarifa ya
maendeleo ya watu nchini Tanzania (THDR), Dr. Tausi Kida akifuatilia kwa
makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Prof. Sylvia Temu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano huo. Kulia
ni Gelase Mutahaba kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kushoto ni Prof.
Bertil Tungodden kutoka nchini Norway na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini
ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa pili kushoto).
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, mabalozi, taasisi mbalimbali za serikali waliohudhuria mkutano
huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar.
*SEKTA ZA MADINI ,UMEME NA KILIMO ZAKUZA PATO LA TAIFA.
Mkurugenzi
wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la
Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bw. Oswald
Ruboha (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara
ya Kilimo na Dkt. Stephen Kirama (kushoto), Mhadhiri wa Uchumi, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
Sekta ya Kilimo,Uvuvi, Viwanda
, Nishati na Madini zimeelezwa kuwa miongoni mwa sekta muhimu
zinazoongoza zaidi katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa hadi
asilimia 7.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2014.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya
uzalishaji nchini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kutumia kanuni
za kimataifa kukokotoa pato la Taifa zinaonyesha kuwa sekta hizo zimetoa
mchango mkubwa wa kukua kwa pato la Taifa kwa asilimia 7.4 kuanzia mwezi Januari hadi Machi, 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.1 za mwaka 2013.
Mkurugenzi
wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke
akizungumzia ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es
salaam amesema kuwa Pato la Taifa katika robo ya mwaka 2014 kuanzia
Januari hadi Machi limekua kwa asilimia 7.4 kutokana na kukua kwa sekta
za Kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi, Umeme na utoaji wa huduma.
Amesema
sekta zilizofanya vizuri katika ukuaji huo ni pamoja na sekta ya
uchimbaji wa Madini, mawe na kokoto ambayo imekua kwa asilimia 8.7
ikilinganishwa na asilimia 1.7 za mwaka uliopita kutokana na kukua kwa
masoko ya uuzaji ya nje ya nchi.
Ameongeza
kuwa sekta uzalishaji wa bidhaa za viwandani imekua kwa asilimia 8.5
kutoka 8.3 huku shughuli za utoaji wa huduma na uchumi zikiwemo za
ukarabati wa magari, pikipiki na vifaa vingine vya majumbani zikikua kwa
asilimia 8.0 kwa robo ya mwaka 2014.
Bw.
Oyuke ameeleza kuwa shughuli za uchukuzi na mawasiliano zimefikia kasi
ya ukuaji wa asilimia 16.5 katika kipindi hicho na kuongeza kuwa huduma
za hoteli na migahawa zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 3.0, huku
shughuli za uendeshaji wa Serikali zikifikia asilimia 5.1, Elimu
asilimia 5.2, huduma za Sfya na shughuli nyingine zikikua kwa asilimia 4.5.
Aidha,
amefafanua kuwa sekta ya umeme katika robo ya mwaka 2014 imekua kwa
asilimia 12.6 ikilinganishwa na asilimia 6 ya mwaka uliopita kutokana na
kupatikana kwa vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme hususan ugunduzi wa
gesi nchini ambao umeondoa tatizo la utegemezi wa umeme wa maji katika
kuzalisha umeme.
“Kwa
kipindi kirefu sekta ya umeme imekuwa na mawimbi kwa kiasi kikubwa ,
umeme wetu umekuwa wa kutegemea maji ya mvua, baada ya juhudi za
Serikali na kugundulika kwa nishati ya Gesi nchini na kupatikana chanzo
mbadala cha nishati tatizo hili limeshghulikiwa sasa sekta hii
imeimarika” Amesisitiza.
Amesema
Tanzania sasa inafanya vizuri kiuchumi katika nchi za Afrika ya
Mashariki kwa kuwa ya pili ikifuatiwa na Uganda, Rwanda na Burundi na
kuongeza kuwa hali ya amani na utulivu iliyopo nchini inaiweka Tanzania
katika nafasi nzuri ya kukua zaidi kiuchumi.
Kwa
upande wake mtaalam wa wa Uchumi kutoka Benki Kuu ya Taifa (BOT) Bw.
Davidi Kwimbere akifafanua kuhusu hali iliyopo ya ukuaji wa uchumi
amesema kuwa imechangiwa na kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji .
Amesema
sekta ya Kilimo na uzalishaji wa mazao imekua kutokana na matumizi ya
mbolea, zana bora za kilimo, mbegu bora, madawa na kufafanua kuwa endapo
juhudi zaidi zitaendelea kufanywa na wananchi kwa kuingia katika
shughuli mbalimbali za uzalishaji uchumi utaendendelea kuonekana kwa mtu
mmoja mmoja.
Amefafanua kuwa maendeleo katika nchi yoyote yanachukua muda na kutoa wito kwa nchi za Afrika kuendelea kujifunza na
kufafanua kuwa nchi zote zilizopiga hatua kimaendeleo mpaka kufikia
asilimia 15 ikiwemo China iliwachukua miaka 20 kuondoa umasikini.
Amesema Tanzania inayo nafasi nzuri kukua kiuchumi kutokana na kuendelea kuimarika kwa miundombinu na ukuaji wa sekta za ujenzi, Nishati, madini, Viwanda, umeme , kilimo na uvuvi hali inayochangia kuongezeka kwa uwekezaji.
No comments:
Post a Comment