Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni
ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wadau na wananchi wakijipanga tayari
kuanza kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo mbalimbali ya katikati
ya jiji iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
ikiwa ni awamu ya kwanza kwa mwaka huu kabla ya kuelekea kwenye kata
nyingine mbili zilimo ndani ya manispaa ya Ilala wakishirikiana na
wananchi.
Na Mwandishi wetu
WILAYA ya Ilala imeanzisha kampeni
ya wiki tatu ya usafi katika maeneo yaliyopo katikati ya Jijini la Dar
es salaam kwa lengo la kutoa elimu na kuyaweka maeneo hayo safi na
salama.
Kampeni hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa juma katika eneo la Kisutu na Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi .
Akizundua kampeni hiyo alisema bila
suala la usafi kufanyiwa kazi, wageni wataona kwamba mambo katika Jiji
la Dar e s salaam ni hovyo hasa ikizingatiwa kwamba kati ya jiji ndio
sebule ya Jiji.
Kampeni hiyo inayosimamiwa na
kampuni yenye dhamana ya usafi katika eneo hilo la kati ya Green Waste
Pro Limited inashirikisha wananchi kwa lengo la kuwafanya wawe washirika
wa usafi kwa kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu.
Mkuu huyo wa wilaya pamoja na
kushukuru wananchi na wanafunzi wa shule ya Kisutu waliofika katika
kampeni aliwataka viongozi kujipanga kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa
endelevu na yenye mafanikio.
Kampeni hiyo inafanyika katika kata ya Kivukoni, Kisutu na Mchafukoge.
Pamoja na Mkuu huyo wa wilaya kusema
kwamba kampeni hiyo ni chachu kwa kata za pembezoni za kujali usafi
amewataka wananchi kuwa washiriki kw akuhakikisha hawatupi uchafu hovyo.
Naye Naibu Meya na Diwani wa Kisutu
Kheri Kessy alisema kazi ya usafi inakabiliwa na changamoto kubwa hasa
kutokana na kuvuja kwa chemba za maji machafu na wananchi kutupa taka
hovyo.
Alisema wananchi na hasa wapiti
njia kama wakijifunza kutupa uchafu maeneo wanayotakiwa watakuwa
wamesaidia sana kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu na pia kufanya
maeneo yapendeze.
Alisema wananchi wa kata yake ya
Kisutu ni waelewa tangu kuanza kwa kampeni hizo miaka miwili iliyopita
lakini wapiti njia wamekuwa wakivuruga utaratibu wa usafi.
Aliwataka wakazi wa dare s salaam
kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha hawatupi taka hovyo na kuanza
kuuchukia uchafu kutoka katika majumba yao hadi wanakotembea.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro
Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na
baadhi ya madiwani wa kata tatu zilizomo ndani ya manispaa ya Ilala na
watendaji wa halamshauri ya manispaa ya Ilala wakati wakimsubiri mgeni
ramsi kuzindua kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo yanayozinguka
manispaa hiyo wakianzia katikati ya jiji. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa
Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena.
Kampuni inayoendesha kampeni hiyo ya
Green Wate kupitia kwa meneja wao Abdallah Mbena amesema kwamba kuna
maendeleo makubwa katika kamepni za kuweka Jiji safi na safari hii
wamewaalika wenzao kutoka Segerea na Upanga ili waone njia wanazotumia
kuweka maeneo yao yenye dhamana safi na ya kupendeza.
Mbena alisema changamoto kubwa
zinazokabili juhudi za kuweka maeneo safi ni upungufu wa usimamizi
katika sheria kwani wengi hawakubali kuzitii.
Alisema kama wangelizitii
kungelikuwa na usafi kila siku. Kwani wengine wamekuwa wakifika katika
majengo yao na kuyasafisha na kutupa uchafu barabrani wakati wafagiaji
wameshafanyakazi yao usiku.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya
kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo
(katikati) na Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro
ltd Bw. Abdallah Mbena wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na vyombo
vya habari kuhusiana na kampeni hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari na wananchi wa Kata
ya Kisutu muda mfupi kabla ya kuzindua kampeni ya chukia uchafu katika
kata tatu za wilaya hiyo. Kata hizo ni Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni.
Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy na kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi iliyopewa zabuni ya kusafisha
Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,
Kheri Kessy akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa rai kwa
wananchi wa kata hizo kuunga mkono kampeni hiyo yenye lengo la
kung'arisha vitongoji vya manispaa ya Ilala na wengine waige kutoka
kwao.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
wasichana ya sekondari Kisutu na wafanyakazi wa Green Waste Pro ltd.
waliojumuika na kampuni ya Green Waste Pro Ltd kuunga mkono kampeni hiyo
ya iliyopewa jina na Mkuu wa wilaya ya Ilala ya "Chukia uchafu".
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafi
iliyopewa zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Bw.
Anthony Mark Shayo kwenye picha ya pamoja na watendaji wa manispaa ya
Ilala na madiwani wa kata hizo tatu.
No comments:
Post a Comment