Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa
Namibia muda mfupi kabla ya kuhudhuria mkutano Wake wa Marais na Wakuu
wa Nchi za Afrika kuhusu masuala ya saratani ya shingo ya kizazi,
saratani ya matiti na saratani ta tezi la kiume (prostate cancer) huko
New York tarehe 24.9.2014. Mkutano huo umefadhiliwa na Umoja wa Mataifa
kwa kushirikiana na Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative ya
nchini Nigeria.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kikao cha Wake
wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kichozungumzia masuala ya saratani
ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi la kiume
huko New York tarehe 24.9.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Penehupifo Pohamba
mara baada ya kuhutubia mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za
Afrika uliofanyika New York tarehe 24.9.2014. Katikati ni Princess Nikky
Onyeri, Mmiliki wa Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative and
Forum of African First Ladies Against Cervical,Breast and Prostate
Cancer ya Nigeria.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika
wakimsikiliza Mama Salma alipokuwa anahutubia mkutano huo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Princess
Nikky Onyeri (kushoto) na Gill Bishop mara baada ya mkutano. PICHA NA
JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment