Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akionozana na akina mama wa
jamii ya kimasai waliobeba maji waliyoyateka baada ya mbunge huyo
kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, Bagamoyo
mkoani Pwani jana. Kisima hicho pamoja na lambo la kunyweshea mifugo
vimejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. Kushoto ni
Kiongozi wa mradi huo, Joseph Chagama na nyuma yake ni Askofu wa Kanisa
la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana.
Ridhiwani
Kikwete akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho.
Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark
Malekana.
Ridhiwani
akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa jamii ya kimasai baada
ya kuzindua kisima hicho.
Ridhiwani
Kikwete akifungua maji ikiwa ni ishara ya kuzindua lambo la kunyweshea
mifugo katika Kijiji cha Mbala kinachokaliwa kwa asilimia kubwa na jamii
ya wafugaji
Ng'ombe wakitoka kunywa maji kwenye lambo hilo
Watoto wa kimasai waonja maji ya kwenye lambo baada ya uzinduzi
Kwaya
ya Amkeni ya Kanisa la Wasabato la Mbala, ikitumbuiza wakati wa hafla
ya uzinduzi wa kisima cha maji uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, mkoani
Pwani jana. Kanisa hilo limejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya
sh. mil. 76.
Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia) akishiriki katika maombezi
Kwaya ya Kanisa la Wasabato la Manzese wakimwimbia bwana wakati wa hafla hiyo. . PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment