SIKU
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali
imewadia ambapo kesho Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa patakuwa
hapatoshi wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua
nafasi.
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli.
Akizungumza
na Centre Spread, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kuwa
maandalizi yote yameshafanyika na tayari mkali wa muziki kutoka Nigeria
anayetamba na ngoma ya Johnny, Yemi Alade ameshatua nchini,
kinachosubiriwa ni burudani mwanzo mwisho.
“Kila
kona ya burudani imeshakamilika hivyo kama wewe ni mpenzi wa ndondi
kuna ngumi kati ya mabondia Mada Maugo dhidi ya Thomas Mashali, JB dhidi
ya Cloud 112, Said Memba dhidi ya Khalid Chokoraa na wengineo.
Navy Kenzo.
“Wapenzi
wa Bongo Fleva, kutakuwa na mfalme wao, Ali Kiba akiwa sambamba na
mastaa kama Shilole, Madee, R.O.M.A, Meninah, Navy Kenzo, Scorpion
Girls, Juma Nature na wengine kibao,” alisema Maloto na kuongeza:“Kwa
wale wapenzi wa soka basi watakutana na mechi kabambe kati ya Wabunge
Mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga, Azam Fc dhidi ya Mtibwa,
Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na wengine wengi.”
Ally Kiba.
Maloto
aliongeza kuwa jukwaa litashambuliwa pia na wanamuziki wa nyimbo za
Injili kama Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Angel na wengine wengi.
Tamasha la Usiku wa Matumaini linatarajiwa kuanza kesho saa 5 asubuhi
hadi saa 6 usiku ambapo wapenzi wa burudani watainjoi mambo yote kwa
kiingilio cha shilingi elfu 5 tu.
No comments:
Post a Comment