Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleimkan
Said Suleiman (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi
madawati hayo. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina
Kasyupa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Eva Mbena.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleimkan
Said Suleiman (katikati), akipeana mkono na dada mkuu wa shule hiyo,
Celina Dismas baada ya kukabidhi madawati hayo. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa
shule hiyo, Christina Kasyupa.
Mjumbe
wa Bodi ya Shule hiyo Emanuel Mlangali (kulia), akiwa na walimu wa
Shule jirani. Kutoka kushoto ni Mwalimu Saum Mwabi wa Shule ya Msingi
Mwale na Mwalimu Anna Kyoma.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Christina Kasyupa akizungumza katika hafla hiyo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa kuimba kwenye sherehe hiyo.
Kikundi cha Makhirikhiri cha shule hiyo kikitoa burudani.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleimkan
Said Suleiman akisalimiana na wanafunzi wa shule hiyo.
Dotto Mwaibale wa mtandao wa www.habari za jamii.com
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imetoa msaada wa madawati 100 kwa
Shule ya Msingi ya Yombo iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam
ili kukabiliana na changangamo ya madawati shuleni hapo.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi madawati hayo Dar es Salaam leo aasubuhi
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Suleimkan Said Suleiman
alisema msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya TAA kwa shule hiyo
walioitoa mwaka jana.
"Kazi
hii tunayoifanya ni kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa na kudumisha
ujirani mwema uliopo kati ya shule yenu na Kiwanja cha chetu cha ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)" alisema Suleiman.
Alisema
mwaja jana TAA ilitoa ahadi kwa shule hiyo ya kuwapa sh.milioni 10 ili
ziwezekusaidia kupunguza tatizo la madawati ahadi ambayo wameitimiza
jana kwa kutoa madawati hayo yenye thamani ya sh.milioni 10.
Suleiman
alisema msaada huo utakuwa kwa kamati ya shule hiyo na kuongeza
jitihada za kuboresha zaidiufaulu kwa shule hiyo na wanafunzi kuhudhuria
shuleni bila ya kukosa kwa faaida yao na Taifa kwa ujumla.
Katika
hatua nyingine Suleiman alitumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa shule
hiyo pamoja na wanafunzi hao kuyatunza madawati ili yaweze kusaidia na
vizazi vingine.
Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Christina Kasyupa aliishukuru TAA kwa msaada huo
kwa shule hiyo na kuwa wameupata kwa wakati muafaka kutokana na
changamoto waliyokuwa nayo ya ukosefu wa madawati.
Shule
ya Msingi ya Yombo ilianzishwa mwaka 1962 na imefanikiwa kufaulisha
wanafunzi kwa asilimia 85 kwenda sekondari mwaka2013 na kupata cheti cha
ugaguzi daraja A na sasa ipo katika Mpango wa Serikali wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya elimu.
No comments:
Post a Comment