DINI YETU :MH.FREDERICK SUMAYE AZINDUA ALBAMU MPYA YA ROSE MUHANDO JIJINI DAR - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 4 August 2014

DINI YETU :MH.FREDERICK SUMAYE AZINDUA ALBAMU MPYA YA ROSE MUHANDO JIJINI DAR

  Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,mara baada ya kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na wapenzi wa nyimbo hizo za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar jana.
Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akifungua kasha lenye CD, wakati akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando wakishuhudia tukio hilo.
Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.
 Baadhi ya Wadau wa Muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.
 Sehemu ya umati ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na  skwadi lake jukwaani wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu  Mstaafu,Mh Frederick Sumaye.
 Rose Muhando akiimba kwa hisia
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi huo
 Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho,Upendo Kilahilo,akiimba jukwaani.
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Sara K akiimba
 Waziri Mkuu  Mstaafu,Mh Frederick Sumaye na wadau wengine wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la Shikilia Pindo la Yesu.

No comments:

Post a Comment