Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd
Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal
Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni,
Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa
hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya
Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.
Wafuasi wa CCM na Chadema
wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM
walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akihutubia
na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia
katika mkutano huo.
Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa
Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali
lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika
aeleze ni jitihada hani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua
changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto)
na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), wakitofautiana
jukwaani wakati Makalla akiamuru polisikuwatoa wafuasi wa Chadema
waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM JUU YA
MAJI, HUKU mNYIKA AKITAKA WAENDEE KUZOMEA AKIDAI KWAMBA WAZIRI
HAKUFANYA HAKI KWANI YEYE ALIPOKUWA AKIZOMEWA NA WANA CCM HAKUWACHUKULIA
HATUA KAMA HIYO KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA
SHULE YA MAVURUNZA, KATA YA SALANGA
Mfuasi wa CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, EvaSinare
(katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri
wa Maji, Amos Makalla 9kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema
Mbunge wa Jimbola Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara
Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambapo
aliwahakikishia wananchi wa jiji la Dares Salaam kwamba ifikapo
mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa baada ya
kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi wake
umeanza sasa.
Makalla akipata maelezo kutoka
kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba,
Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam
na Pwani.
Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya Kibamba.
Mwalimu wa Shule ya Msingi ya
Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji
yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo
Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Maji Safi na Taka Dares Salaam, (Dawasco), Jackson Midalla akijibu moja
ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemvu
wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa maji katika kata hiyo.
Wafuasi wa CCM na Chadema
wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwakwenye magari eneo
la Kibamba. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment