AJALI YA BASI : WATU ZAIDI YA 17 WAFARIKI KWENYE AJALI KATI YA BASI LA MORO BEST NA LORI LA MIZINGO, DODOMA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 30 July 2014

AJALI YA BASI : WATU ZAIDI YA 17 WAFARIKI KWENYE AJALI KATI YA BASI LA MORO BEST NA LORI LA MIZINGO, DODOMA

Miili ya  abiria  waliokuwa katika basi la moro Best
Wananchi  na baadhi ya  wasafiri  wakitazama  ajali mbaya ya   lori na basi la Moro Best leo 
basi la Moro Best  likiwa limeharibika vibaya  kufuatia ajali  mbaya  iliyotokea  eneo la Pandambili mapema  leo 
Lori la kampuni ya  Tanesco  likiwa  limejaza miili ya  watu  waliokufa katika ajali  hiyo  leo 

HUKU sherehe za sikukuu ya Idd -El Firt imeelekea ukingoni Taifa limepatwa na msiba mkubwa baada ya watu zaidi ya 17 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Moro Best kupata ajali mbaya eneo la Pandambili katikati ya Dodoma na Morogoro .

 Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima.co.tz kutoka eneo la tukio mmoja kati ya mashuhuda wa ajali hiyo Joseph Mtweve  alisema kuwa tukio limetokea eneo hilo la Pandambili wakati lori lililokuwa limebeba mabomba kutoka Morogoro kwenda Dodoma kujaribu kulipita gari jingine mbele eneo ambalo lina kona na hivyo kugongana na basi hilo uso kwa uso. 

 Alisema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Dodoma kuelekea mkoani Morogoro na kuwa katika ajali hiyo watu zaidi ya 12 walikufa papo hapo na wengine watano wanasadikika kufia njiani wakati wakikimbizwa Hospitali kwa matibabu zaidi.

Miongoni mwa  waliopoteza maisha katika ajali  hiyo inadaiwa pamoja na  dereva wa  basi hilo japo  jitihada za kupata  undani  wa  tukio  hilo  kupitia kwa  jeshi la polisi  zinaendelea kufanyika na mtandao huo

No comments:

Post a Comment