Mtanzania
mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya “Woman with
Altitude” iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP),
Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jana
kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa
Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa
Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa
Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Beda Msimbe, Zanzibar
UNAWEZA
kudhani kamba kila aliyefanikiwa amezaliwa na kijiko cha fedha, yaani
amezaliwa katika eneo lenye hali shwari na kitanda chake ni mayai ya
dhahabu, kumbe sivyo kabisa.
Hili linajadliwa kwa undani katika sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with Atitude.
Sinema
hii ambayo inaoneshwa katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe
imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutambua
kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa migogoro inayowakuta na kwa
kupitia elimu.
Women with Altitude inazunguka katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini.
Baada
ya kufanikiwa kupanda mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal
waliamua kupanda milima mingine mirefu katika mabara mbalimbali wakiwa
na lengo la kutoa ushawishi kwa wanawake na wasichana duniani kote
kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni magumu na hayawezekani.
Machi
2013,wanawake hao walipata ushosti kutoka kwa wanawake wa Kiafrika wane
akiwemo muigizaji wa Afrika kusini Hlubi Mboya,ambaye anatambulika sana
kwa kuigiza nafasi ya mtu anayeishi na VVU kama Nandipha kwenye
Isidingo kupanda mlima mlima mkubwa wa bara la Afrika, Mlima
Kilimanjaro.
Afisa
Habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na filamu iliyopewa
jina la “Women with Altitude” ambapo ndani yake wameshirikishwa
wasichana wa kitanzania wawili na imefadhiliwa na shirika hilo
imeonyeshwa jana ndani ya viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar
linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF 2014.
Tofauti ya utamaduni na mazingira kwa wanawake wote 11 ilikuwa pia ni ishara ya matatizo waliyokumbana nayo katika maisha yao.
Filamu
hii ya Women with attitude inaonesha matatizo ya wanawake hao 11
waliokuwa wakikumbana nayo katika maisha yao yote, na nafasi ya elimu
katika kuwasaidia kufika pale walipo kwa leo.
Wanawake
hawa wanaonekana wakikabiliana na Mlima Kilimanjaro, wakiangalia maisha
ya wenzao na kuwashawishi katika kutokata tama na badala yake kutumia
changamoto kuleta maisha yenye hadhi ya aina yake.
Ofisa
habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumza katika mahojiano alisema kwamba
taarifa iliyomo ndani ya sinema hiyo ni ujumbe tosha kwa vijana na
wanawake kuhusu ukweli wa maisha na namna ya kuyabadili.
Baadhi
ya waandishi wa habari, waigizaji wa filamu na Producers waliohudhuria
mkutano huo ndani ya hoteli ya Doubletree by Hilton.
Mmoja
wa washiriki wa sinema hiyo kutoka tanzania, Ashura Kayupayupa alisema
kwamba alipoteza baba yake akiwa na umri wa miaka minane, lakini
mafanikio yake yote yametegemea jinsi alivyokabiliana na shida zilizopo.
Baba yake alikufa kwa ajali ya gari.
Alisema
baada ya baba yake kufa hali ilikuwa mbaya katika familia kwa kuwa mama
yake alikuwa anamtegemea baba yake kwa kila kitu, wakajikuta hawana
namna ya kufanya.
Ashura
ambaye amezaliwa miaka 24 iliyopita anasema kwamba kutokana na vikwazo
ambavyo amekumbana navyo toka baba yake kuondoka vilimfanya kuwa na
mawazo mengine ya maisha.
Alisema baada ya baba yake kufa alienda kulelewa na ndugu wa baba yake ambao walikuwa wanamvuruga na kumtesa.
Ashura
Kayupayupa akibadilishana mawazo na mbunifu wa mavazi mkongwe Farouk
Abdallah mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Alisema
licha ya kuteswa alikuwa anaenda shule kama kawaida na kujitahidi
kusoma.Amesoma shule ya msingi Temeke, kisha sekondari ya Kijitonyama
kabla ya kuenda al Haramain kumaliza kidato cha sita na kwenda Chuo
Kikuu cha Tumaini kuchukua sheria.
Kwa
sasa yeye ni mwanasheria na anasema kwamba kuacha kusoma kwa sababu ya
kuteswa ni upuuzi kwani ndio zinaua fursa ya kujitambua duniani na
kujiendeleza.
Alisema
ni vyema wanawake wasikimbilie kulalamika kwamba hawakusoma kwa sababu
ya mateso au wazazi wao kufa. Alisema ni vyema mtu kuwa na malengo na
kujifunza vitu hata kwa kujitolea mpaka kieleweke.
Ashura Kayupayupa akipiga picha ya kumbukumbu na mbunifu wa mavazi visiwani Zanzibar Farouk Abdallah.
No comments:
Post a Comment