SEKTA YA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI: WADAU WA SEKTA YA MAWASILIANO KUTOKA (EACO) WAJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI , JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jun 2014

SEKTA YA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI: WADAU WA SEKTA YA MAWASILIANO KUTOKA (EACO) WAJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI , JIJINI ARUSHA


IMG-20140618-WA0010
Mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi  ambaye pia ni  mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Kenya.
IMG-20140618-WA0004
 Mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Uganda Patrick Mwesigwa
IMG-20140618-WA0001
 Mkurugenzi wa  Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema
IMG-20140618-WA0005
Balozi Joseph Bangurambona wa Burundi akiongea juu ya mkutano huo
IMG-20140618-WA0003
Wadau wakifatilia mkutano huo, jijini Arusha
IMG-20140618-WA0011
Kulia Pamela Mollel wa jamiiblog na Jusline Marko wa gazeti la Siha Leo
 
Na mwandishi Wetu - Arusha

Wadau  zaidi ya mia moja kutoka taasisi za mamlaka ya mawasiliano Afrika Mashariki (EACO} wamekutana jijini Arusha ili kuangalia namna ya kuweza kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo muhimu ya mawasiliano.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi  ambaye pia ni  mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Kenya alisema kuwa mkutano huo unalenga kujadili  changamoto zilizobainishwa na wadau wa sekta hiyo kuhusu vikwazo ambavyo vinakwamisha mbalimbali  usambazaji wa mawasiliano kwa nchi hizo.
 
Wangusi alisema kuwa  sekta ya mawasiliano ina vitengo mbalimbali ikiwemo posta,mawasiliano ya simu na utangazaji na mitandao ya kijamii(internet) ambayo bado inakabiliwa na changamoto nyingi  zinazohitaji juhudi za wadau wa sekta hiyo ili kuwafikia watumiaji.
 
Aidha alibainisha kuwa huduma ya posta bado inakabiliwa na changamoto ya anuani makazi ili kuwawezesha watumiaji  wanaoutumia huduma hiyo iweze kuwafikia kwa haraka kama zilivyo huduma nyingine.
 
Hata hivyo wangusi aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa ni mawasiliano ya huduma za simu katika nchi za Afrika mashariki ambapo mbali na watoa huduma kupata faida kubwa lakini pia wanawatoza watumiaji gharama kubwa hivyo kupelekea watumiaji kutoka nchi moja hadi nyingine kushindwa kumudu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema alisema lengo ni kuangalia kuwa mawasiliano yanawafikia watumiaji  na kufaidi huduma hiyo ya simu,internet,utangazaji na maswala ya posta.
 
Alisema kuwa mawasiliano hayafahamu mipaka hivyo ni wajibu wa watoa huduma kutoa huduma bora na nafuu ili watumiaji waweze kuwasiliana na kuungana pamoja katika maswala mbalimbali likiwemo swala la ukuaji wa uchumi.
 
Mkutano huo umekutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano kutoka nchi tano zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki lengo likiwa ni kutoa majibu ya changamoto hizo ambapo mwenyeji wa mkutano huo ni Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad