Majaji wakiwa kazini katika Shindano lililofanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza.Picha na Maktaba.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions, Dar Es Salaam
Shindano
la Tanzania Movie Talents (TMT) Kwa KAnda ya Pwani limemalizika leo
Mkoani Dar Es Salaam mara baada ya washindi watano watakaoiwakilisha
Kanda hii katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane
kupatikana katika Ukumbi wa Makumbusho na hatimaye washindi hao
Kukabidhiwa shilingi laki tano taslimu.
Shindano
hili lilianza tarehe 30 Mei 2014 na kusimama kwa Muda kutokana na Msiba
wa George Tyson ambae alikuwa ni mzazi mwenza wa jaji Yvonne Cherry au
Monalisa. Katika Kuungana nae katika kipindi kigumu alichopitia Timu
nzima ya TMT ilibidi kusimamisha Shindao hilo Kwa Muda hadi pale Msiba
kumalizika, na Baada ya Msiba kumalizika Shindano hili liliendelea tena
mnamo tarehe 15 June 2014 na kufikia tamati leo kwa Washindi watano
Kupatikana.
Kanda
ya Pwani inahusisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar Es Salaam ambapo
takribani washiriki 300 waliweza kujitokeza kwaajili ya kushiriki
shindano hili kwa Kanda ya Pwani.
Washindi
watano waliopatikana katika Kanda ya Pwani wataungana na Washindi
wengine kutoka Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na
Kaskazini ambao walishapatikana kwaajili ya kuingia kambini ambapo
wawakilishi hao wa kanda hizo watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu wa
Sanaa wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Kutoka Chuo Cha Sanaa cha
Bagamoyo na hatimaye wataendelea na mchujo ambapo Mshindi mmoja
ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali
kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.
Vilevile
vipindi vya Shindano hili vinarushwa katika kituo cha runinga cha ITV
siku ya Jumamosi saa 4 Usiku na Marudio yake ni Saa 10 Jioni siku ya
Jumapili na Jumatano ni saa 5 usiku.
Na
Jumamosi ya Wiki kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa muda ule ule wa
Saa 4 Usiku siku ya Jumamosi na marudio yake siku ya Jumapili saa 10
Jioni na Jumatano saa 5 usiku.
Washindi
wa Kanda zote wanatarajia kuwasili katika Nyumba ya TMT hivi karibuni
kwaajili ya Kuanza kambi kwaajili ya safari ya kuwania Shilingi Milioni
50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Vilevile
katika Fainali hiyo washindi kumi bora watakuwa chini ya Kampuni ya
Proin Promotions ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano hili na
hatimaye wataweza kufanya kazi ya pamoja na hatimaye kunufaika na Kazi
hiyo.
Shindano
hili la Tanzania Movie Talents (TMT) lilianza safari zake za kusaka
Vipaji katika Kanda ya Ziwa na kuendelea na zoezi hilo kanda ya Kati,
Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini na hatimaye safari hizo
zimefikia tamati leo mara baada ya washindi watano kupatikana kutoka
Kanda ya Pwani.
No comments:
Post a Comment