Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Msiba wa msiba wa msanii
maarufu wa filamu ya vichekesho hapa nchini,Marehemu Saidi Ngamba “Mzee
Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam
Juni 9, 2014.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa
wakati walipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho
Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga
jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014
Mama
Salma Kikwete akimpa pole mjane wa Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Smal”
wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo maarufu wa filamu za
vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam Juni 9, 2014.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amejumuika na waombolezaji mbali mbali
kwenye Msiba wa msanii maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa
marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam Juni 9, 2014.
Rais Kikwete akisaini Kitabu cha Maombolezo.
Dua zikiendelea kusomwa kumuombea Marehemu Said Ngamba "Mzee Small".
MC Mkwere akiongoza shughuli ya Msiba huo.
Waombolezaji Msibani.
Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba akionekana ni mwenye Majonzi sana.
Mmoja kati ya watu waliofanya kazi nyingi na Marehemu Mzee Small,Bwana Tupatupa akiongea na vyombo vya habari.
Rais Kikwete akiwaaga waombolezaji msibani hapo.
Mama Salma Kikwete akiondoka msibani hapo baada ya Kuhani msiba huo.
Waombolezaji msibani.
Jeneza likipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya Mazikoni.
Msafara
wa magari na waendesha Bodaboda wakiwa katika barabara ya Segerea
Kinyerezi wakati wakielekea Makaburi ya Segerea kwaajili ya Kumpumzisha
Kwa Amani Mkongwe wa Sanaa ya Vichekesho Nchini Said Ngamba almaarufu
Mzee Small
Gari
lililobeba Mwili wa Marehemu Said Ngamba aka Mzee Small (la kwanza)
likiwa limesimama kwaajili ya Vijana kuubeba Mwili wake hadi kwenye
Makaburi ya Segerea jioni Hii
Vijana wakishusha jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small kwaajili ya kuelekea kwenye Makaburi ya Segerea
Vijana
wakiwa wamepanga mstari kuanzia Barabara ya Segerea Kinyerezi hadi
makaburini kwaajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small
Watu mbalimbali wakisubiri Mwili wa Marehemu kuwasili katika makaburi ya Segerea
Mwili
wa Marehemu Mzee Small ukitolewa kwenye jeneza tayari kupumzishwa
katika Nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Segerea.
Watu
mbalimbali wakiwasili kwenye makaburi ya Segerea kwaajili ya kumzika
Mzee Small. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
No comments:
Post a Comment