..................................................................................................
ASKARI wa usalama barabarani nchini wamepewa rungu la kuwakamata madereva wa mabasi ya abiria na magari mengine ambayo yatapatikana yakivunja sheria ya uchafuzi wa mazingira ya kusimamisha mabasi ili abiria waweze kuchimba dawa porini kinyume na taratibu.
Agizo hilo limetolewa leo wakati wa semina elekezi ya mikakati ya kuthibitia ajali na uboreshaji wa huduma ya usafiri ,iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu( SUMATRA)makao makuu kwa askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa.
Mwanasheria mkuu wa SUMATRA Bi Leticia Mutaki alisema kuwa kisheria kuchimba dawa ovyo ni kosa na hivyo lazima askari wa usalama barabarani kote nchini kuhakikisha wanasimamia sheria hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wale wote wanao vunja sheria hiyo.
Alisema kuwa tarayi SUMATRA ilitangaza vituo vya uchimbaji dawa kwa barabara zote nchini na wamili wa mabasi hayo wamepewa nakala yake hivyo ni lazima kuzingatia sheria hiyo na kusimamisha basi eneo husika ambao wametengewa .
Huku kwa upande wake mkuu wa uparesheni barabarani kutoka Sumatra Person Mpina alisema kuwa mbali ya askari hao kuwabana madereva ambao wanavunja sheria kwa kuchimba dawa popote bado askari hao wanapaswa kuchukua hatua kwa madereva wa mabasi ya nje ya nchi ambao wamekuwa wakikiuka sheria kwa kufanya biashara ya kupakia abiria wakiwa ndani ya nchi .
Alisema kisheria mabasi ya nje hayapaswi kupatika abiria ndani ya nchi isipokuwa magari hayo yanaruhusiwa kushusha abiria pekee.
Kuwa mabasi yaliyosajiliwa kwa namba za usajili za Kenya ,Kampala ,Zambia na nchi nyingine wanapaswa kupatika abiria wanapoingia katika nchi husika na sio kupakia abiria ndani ya nchi.Kuhusu mabasi ya masafa marefu yaendayo mikoani kuingia ama kutoingia katika stendi ya wilaya alisema kuwa si lazima kwa mabasi ya mikoai kuingia katika stendi za wilaya na kuwa mabasi hayo yanaruhusiwa kuingia stendi za mikoa pekee na si vinginevyo .
"Suala ambalo tunaliangalia hapa na tutalitolea majibu ni juu ya stendi ya ipi ya mkoa kati ya Ipogolo na ile ya Iringa mjini ....kwani kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa wa stendi ya mkoa katika mkoa wa Iringa ambapo wengi wao wanatumia stendi zote mbili ya Ipogolo na Miyomboni kama stendi kuu"
Japo alisema abiria anayohaki ya kushushwa katika stendi ya mkoa na si vinginevyo na kuwa kitendo cha madereva wa mabasi ya mikoani kuwashusha abiria Ipogolo na kuwafanya kukodi Taxi kuja mjini Iringa ni kosa kubwa na iwapo abiria ataamua kuchukua hatua za kisheria lazima dereva achukuliwe hatua.Picha na Francis Godwin -Iringa
No comments:
Post a Comment