KOMBE LA DUNIA : UHOLANZI (NETHERLANDS) YAFUZU BAADA YA KUICHAPA AUSTRALIA 3 - 2 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jun 2014

KOMBE LA DUNIA : UHOLANZI (NETHERLANDS) YAFUZU BAADA YA KUICHAPA AUSTRALIA 3 - 2

Rocket: Van Persie smashes a powerful strike into the roof of Australia's net to make it 2-2
Roketi ya Uholanzi: Van Persie akiisawazishia bao la pili Uholanzi 
Jumping for joy: Manchester United striker Van Persie leaps into the air to celebrate his goal
Akiruka kwa furaha: Mshambuliaji wa Manchester United ,  Van Persie akishangilia bao lake la tatu katika fainali za mwaka huu za kombe la dunia.

Comeback complete: Holland substitute Memphis Depay scores from outside the box to make it 3-2


Aliingia kumaliza kazi!:  Memphis Depay akitokea benchi amefunga bao la tatu kwa shuti la mbali na kuipa ushindi wa mabao 3-2 Uholanzi.
HATA kama Louis van Gaal alianza kufunga, lakini haikuwa mechi ya kukaa kwenye kiti. Ulikuwa mchezo mgumu kwake kutokana na uimara wa Australia, lakini dakika za mwisho zimemalizika kwa Uholanzi kushinda mabao 3-2.
Bao la kusawazisha alilofunga Timu Cahil liliwashitua Waholanzi ambao waliokuwa wanashangilia bao la Arjen Robben, lakini kabla hawajakaa wakashangaa nyavu zao kutikishwa.
Australia ambao wako kiwango cha chini kuliko timu zote zinazoshiriki kombe la dunia mwaka huu, walifanya shambulizi la kushitukiza na kufunga goli bora. Pia walijiamini, walikuwa na mipango na kuwayumbisha wana fainali hao wa 2010 nchini Afrika kusini na wababe wa mabingwa Hispania katika mchezo wa kwanza ambao walishinda mabao 5-1.
Bao la kwanza la Uholanzi lilifungwa na Arjen Robben, lakini Australia wakasawazisha kupitia kwa Tim Cahil. 
Autralia waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Mile Jedinak kwa mkwaju wa penati, lakini Robin Van Persie aliisawazishia Uholanzi na hatimaye Memphis Depay akitokea benchi alifunga bao la tatu na la ushindi.
Frustrated figure: Australia goalkeeper Matthew Ryan can only watch as Depay's effort squirms into the back of the net
Mlinda mlango wa  Australia,  Matthew Ryan akiangalia mpira uliopigwa na Depay na kuzama kimiani.
Unstoppable: Australia's Tim Cahill unleashes a left-footed volley to level the score at 1-1
Hazuiliki: Nyota wa Australia, Tim Cahill alifumua shuti kali kwa guu lake la kushoto na kuzamisha gozi kambani na kuufanya ubao usomeke 1-1.
Centre of attention: New York Red Bulls midfielder Cahill wheels away to celebrate his strike
Kiungo wa  New York Red Bulls , Cahill  akishangilia bao lake.

Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vyao. Alama zilizotolewa ni 10.

Kikosi cha Australia (4-2-3-1): Ryan 5; McGowan 7, Wilkinson 6, Spiranovic 6, Davidson 6; Jedinak 7, McKay 6; Leckie 7, Bresciano 6 (Bozanic 51 6), Oar 6 (Taggart 77 ); Cahill 6 (Halloran 69 6)

Kadi ya njano: Cahill
Mfungaji wa Goli: Cahill, Jedinak (pen)
Kikosi cha Holland (3-4-1-2): Cillessen 6; Vlaar 5, De Vrij 6, Martins Indi 6  (Depay 45 8); Janmaat 5, De Guzman 6 (Wijnaldum 78 6), De Jong 6, Blind 6; Sneijder 6; Van Persie 6 (Lens 87 6), Robben 6
Kadi ya njano: Van Persie
Wafungaji wa magoli: Robben, Van Persie, Depay
Mwamuzi: D Haimoudi (Algeria)
Mchezaji bora wa mechi: Depay

Deadly: Holland winger Arjen Robben (right) drives the ball into the bottom corner to give his side the lead
Winga wa Uholanzi,  Arjen Robben (kulia) akiachia bao la kwanza la Uholanzi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad