MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi imewahukumu Raia
wawili wa Kenya, Samweli Saitoti (Saimoo) na Michael Kimani (Mike),
wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua
polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), PC Michael Milanzi mwaka
2007.
Akisoma
hukumu hiyo, Jaji mfawidhi wa mahakama kuu, Jaji Kakusulo Sambo alisema
baada ya kusikiliza na kutafakari ushahidi uliowasilishwa mahakamani
hapo na mashahidi 18 wa upande wa Jamhuri, imeridhika kuwa Jamhuri
ilifanikiwa bila kujenga kesi dhidi ya washitakiwa wote watatu bila kuacha shaka lolote.
Raia hao
ambao walipambana na polisi jijini Arusha kwa saa sita wakijihami kwa
silaha za kivita yakiwamo mabomu ya kurusha kwa mkono na bunduki aina ya
Sub Machine Gun (SMG), walifanya mauaji hayo yaliyoambatana na uporaji
wa Sh239 milioni mali ya Benki ya NMB, Julai 11, 2007.
Pia, Jaji
Kakusulo Sambo wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, amemhukumu Mtanzania,
Calist Kanje kwenda jela miaka mitano kwa kuwasaidia wauaji hao
wasikamatwe na polisi baada ya kufanya mauaji.
Akitoa
hukumu hiyo jana, Jaji Sambo alisema upande wa mashtaka ukiongozwa na
Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya, Stella Majaliwa na Ignas Mwinuka,
umethibitisha mashtaka hayo pasipo shaka.
Jaji Sambo
alisema ushahidi wa mashahidi 18, umethibitisha kuwa raia hao wa Kenya
ndiyo walioshirikiana kwa pamoja, kumuua polisi huyo ambaye taifa bado
lilikuwa likihitaji utumishi wake.
“Kulikuwa na
hoja ya utetezi kuwa hawakutambuliwa kikamilifu lakini PC Naftali
Ashery aliyekuwa lindo na marehemu aliwatambua vilivyo wauaji hao tena
kwa ukaribu,” alisema. Alisema Mahakama imeridhika kuwa maungamo
waliyoyatoa mbele ya walinzi wa amani ambao ni mahakimu waliyatoa kwa
hiari bila kushurutishwa.
Mahakama
imeukataa utetezi wa washtakiwa hao kuwa wakati wa mauaji hawakuwa
nchini, akisema ushahidi wa vinasaba (DNA), umethibitisha walikuwapo
nyumbani kwa mshtakiwa Kanje.
Jaji alisema
kwa kuwa washtakiwa hao walikwenda kwa Kanje na yeye akawasaidia
wasikamatwe na kuwatorosha, hilo ni kosa la kusaidia wahalifu baada ya
kufanya mauaji.
Jaji Sambo
alisema Kanje ndiye aliyeficha gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya
Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR), lililotumika katika ujambazi huo
na kwamba ushahidi wa wafanyakazi wawili wa mshtakiwa huyo,
unathibitisha kuwa ndiye aliyetoa maelekezo kwa dereva wake ili
akalitelekeze gari hilo eneo la Uwanja wa Ndege wa KIA.
Mahakama
hiyo imeamuru kiasi cha fedha, Dola 8,145 za Marekani na Sh1,769,000
walizokutwa nazo raia hao wa Kenya, zikabidhiwe Benki ya NMB, Mwanga
zilikoibwa.
Washitakiwa hao, Samweli Gitau Saitoti na mwenzake Michael Kimani walitiwa hatiani kwa kosa hilo na kufungwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja huku Mtanzania mwengine, mshitakiwa namba 10, Elizabeth Msanze "Bella", mkazi wa kwangulelo mkoani Arusha, akihukumiwa kwenda Jela miaka 7.
Wasitakiwa hao wote kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na shtaka la mauaji
ya kukusudia ya askari polisi katika shauri la namba 6 ya mwaka 2011,
ambapo ilidaiwa kuwa wakiwa na wenzao wengine 9, walishiriki katika
tukio la uporaji na mauaji yaliyotokea, Julai 11 mwaka 2007 katika Benki
ya NMB tawi la Mwanga, wilayani Mwanga , mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment