BURUDANI NA TEKNOLOJIA : MULTCHOICE AFRICA YAKUTANA NA WADAU WAKE NCHINI MAURITIUS - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 25 June 2014

BURUDANI NA TEKNOLOJIA : MULTCHOICE AFRICA YAKUTANA NA WADAU WAKE NCHINI MAURITIUS


Mtendaji Mkuu wa MultChoice Afrika,Nico Meyer akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.Hafla hiyo imekusanya wadau mbali mbali wa MultChoice barani Afrika,ambapo Kampini hiyo itakuwa ikinyesha mambo mbali mbali wanayojihusisha nayo kwenye vipindi mbali mbali vya Televisheni zao za DStV na GoTV.Picha zote na Othman Michuzi.
Meneja wa MultChoice kwa Ukanda wa Afrika Magharibi,Bi. Wangi Mba-Uzoukwu nae alipata wasaa wa kuzungumza machache wakati wa tafrija hiyo ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.
Watangazaji wa Kipindi cha JARA kinachorushwa na DStV, Uti Nwachukwu na Juliet Ibrahim wakiongoza kipindi chao Live ukumbini hapo.
Aki akiingika kwenye kipindi hicho kwa mbwembwe.
Muigizaji wa Filamu toka Nigeria,Ritha Dominic akijibu maswali ya moja kwa moja kutoka kwa wadau mbali mbali wa filamu za Kinigeria waliopo ukumbini hapo.
Mtangazaji wa Redio Clouds FM,Barbara Hassan akiuliza moja ya maswali yake kwa Muigizaji wa Filamu toka Nigeria,Ritha Dominic (picha ya juu).
Mshehereshaji mkuu wa tafrija hii alikuwa ni IK ambaye pia ni muongozaji wa Mashindano ya Big Brother na hapa alikuwa akitaniana na watangazaji wa kipindi cha JARA mara baada ya kumalizika kwa muda wake.


Msanii Nassib Abdul a.k.a Diamond ni mmoja kati ya wasanii saba kutoka barani afrika walioshiriki kutuna na kuimba wimbo wa Africa Rising,pichani ni katika sehemu alioimba Diamond ilipokuwa ikionyeshwa kwenye ukumbi wakati wa kuuzindua wimbo huo.


Wasanii saba kutoka barani afrika walioshiriki kutunga na kuimba wimbo wa Africa Rising (hapa ni Diamond tu ndio hayupo,kutokana na uwingi wa kazi alizonazo)
Burudani mbali mbali zikiendelea.
Meneja Mahusiano wa MultChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kulia) na Mdau Sidi Mgumia (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii wa Filamu kutoka nchini Nigeria,Chinedu Ikedieze (Aki) wakati wa tafrija ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.
Meneja Mahusiano wa MultChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kulia) na Mdau Sidi Mgumia (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watangazaji wa Kipindi cha JARA,Uti Nwachukwu na Juliet Ibrahim. 
Mtaa kwa Mtaa Blog (Othman Michuzi) akiwa na Uti Nwachukwu na Juliet Ibrahim. 
Barbara Bambogi na Ritha Dominic
Taswira ya Kivuli cha ndugu MC.
Shangwe zikiendelea.
Team Tanzania wakiwa ndani ya kiunga cha Mauritius.
Wadau wakipeana mawili matatu wakati wa mkia wa jogoo (cocktail party).
Selfie hiyooo.
Wadau.
Picha zote na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog  na Mdau IK.

No comments:

Post a Comment