JENGO LA BABA WA TAIFA :CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DSM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 25 June 2014

JENGO LA BABA WA TAIFA :CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DSM

 Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu, Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye (kulia) kuhusu picha ya mfano ya mwonekano wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere pindi litakapokamilika.
 Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini Mkapa (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akisalimiana na Mama Maria Nyerere mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) jijini Dar es salaam wakishuhudiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi  Getrude Mongella wakati wa hafla ya uzinduzi wa jingo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kulia) na Mama Maria Nyerere wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu, Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments:

Post a Comment