Katibu Mkuu wa EAC,Dkt. Richard Sezibera |
Mwandishi wetu Arusha
Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera amesema pamoja na mafanikio kadhaa wananchi katika nchi za Afrika Mashariki wanakabiliwa na changamoto ya kupata ajira na mazingira mazuri katika nchi hizo.
Ametoa kauli
hiyo leo wakati wa akifungua mkutano wa kujadili changamoto na fursa
zinazopatikana kwenye nchi za Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.
Dk
.Sezibera amesema mbali na ugumu wa ajira
kwa wananchi kufanya kazi nchini nyingine pia kuna mazingira magumu yasiyorizisha ya
kufanya biashara yanayosababishwa na urasimu kwenye nchi wanachama.
Alisema
wafanyabiashara wanawajibu wa kuzishawishi nchi zao kuweka mazingira mazuri
kwani uchumi wa nchi unategemea sekta binafsi.
Awali
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki(EABC)Felix
Mosha alisema jitihada za makusudi zinatakiwa zichukuliwe ili kurahisisha
mazingira ya kufanya biashara kwenye nchi za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment