Mashabiki wa Manchester City wakiingia uwanjani kushangilia ubingwa wa timu yao.
Wachezaji wa Man City wakishangilia bao lao la kwanza lililowekwa kimiani na Vicent Kompany.
Na Israel Saria
Hatimaye
Manchester City wamefanikiwa kunyakua ubingwa wa England katika siku ya
mwisho ya Ligi Kuu, ambapo walikuwa wakihitaji pointi moja tu kutawazwa
wafalme.
Vijana
hao wa Manuel Pellegrini hawakufanya makosa walipoingia uwanjani
nyumbani dhidi ya West Ham, kwani Samin Nasri na nahodha Vincent Kompany
walihakikisha wanaipatia timu yao mabao, huku ngome ikihakikisha
haivuji.
Wakati
City wakipata ushindi huo, Liverpool waliokuwa wakiunyemelea ubingwa
pia kwa kusubiri kuteleza kwa City, walianza vibaya baada ya
Martin Skirttel kujifunga bao walipocheza dhidi ya Newcastle United na kuwafisha moyo washabiki dimbani Anfield.
Hata
hivyo, Liverpool walizinduka baadaye, wakasawazisha kisha kufunga bao la
ushindi lakini kwa kuzingatia matokeo ya City, Liver walishindwa
kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa huo ambao waliupoteza tangu 1990.
City
walikuwa wakipewa nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa huo, hasa baada
ya Liverpool kuteleza hivi karibuni kwa kukubali kichapo kutoka kwa
Chelsea, kabla ya mechi iliyopita kwenda sare ya 3-3 na Crystal Palace
katika mchezo ambao vijana wa Brendan Rodgers walikuwa wanaongoza kwa
mabao matatu kwa bila.
Nafasi
ya tatu imekwenda kwa Chelsea ambao walianza vibaya mechi yao ya mwisho
dhidi ya Cardiff kwa kutangulia kufungwa, lakini walisawazisha na
kuongeza bao la ushindi katika kulindwa heshima yao. Nafasi ya nne
imeshikwa na Arsenal waliowalaza Norwich 2-0.
Timu
hizo nne ndizo zimeingia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) wakati
Everton waliowafunga Hull mabao 2-0 na Tottenham Hotspur waliowakandika
Aston Villa 3-0 wamefuzu kucheza Ligi ya Europa.
Manchester United wamemaliza msimu kwa sare ya 1-1 na Southampton.
Swansea
waliwakung’uta Sunderland 3-1, West Bromwich Albion wakalala 2-1 kwa
Stoke na Fulham wakatoka 2-2 na Crystal Palace.Norwich wameungana na
Cardiff na Fulham kushuka daraja.
No comments:
Post a Comment