Kocha :Louis Van Gaal .AFP/Photo
KLABU ya Manchester United imemteua Louis
Van Gaal kuwa kocha wake mpya atakayejaza nafasi ya David Moyes
aliyetimuliwa baada ya kuwa kocha kwa miezi 10 pekee.
Mholanzi huyo
ametia saini mkataba wa miaka miaka mitatu na ataanza majukumu yake
uwanjani Old Trafford msimu ujao ikiwa ni baada ya kuongoza taifa lake
kwenye kombe la dunia litakaloanza mwezi ujao nchini Brazil. Msaidizi wa Van Gaal
atakuwa ni Ryan Giggs mkongwe wa klabu hiyo ambaye alitwaa majukumu hayo baada ya kufukuzwa kwa Moyes zikiwa zimesalia mechi tatu msimu
kukamilika.
“Ni furaha
kubwa kwangu na naiona fahari kupata furasa ya kuifundisha mojawapo ya
klabu kubwa duniani Manchester united,” kocha huyo alisema baada ya
uteuzi huo.
Van Gaal
mwenye umri wa miaka 62, amewahi kuzifundisha klabu za Ajaz (Uholanzi),
Barcelona (Uhispania) na Bayern Munich (Ujerumani) ambazo aliziwezesha
kushinda mataji ya Ligi Kuu kabla ya kuajiriwa kuinoa kikosi cha taifa
cha Uholanzi maarufu kama 'oranje'.
Kocha huyo
anategemewa kufufua matumaini ya United baada ya klabu hiyo kumaliza ya
saba msimu huu chini ya Moyes na kuandikisha historia ya kuwa na msimu
mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka 24.
Van Gaal
alishinda mataji mawili ya La Liga akiwa na Barcelona na kujiunga na Bayern aliyotwaa nayo kombe la German Cup
na kufika fainali ya Uefa.
Alijizolea
umaarufu mwaka wa 1995 baada ya kukiongoza kikosi kichanga cha Ajax
kilichojumulisha Clarence Seedorf, Patrick Kluivert na wengineo
kutwa kombe la Uefa kwa kuilaza AC Milan ya Italia.
No comments:
Post a Comment