Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akilakiwa kwa shangwe
alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango katika
Jimbo la Babati Vijijini, mkoani Manyara. Kinana yupo mkoani Manyara kwa
ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi
wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza
kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Tayari kafanya ziara hiyo
katika mikoa ya Tabora na Singida.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akilakiwa kwa shangwe
alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango katika
Jimbo la Babati Vijijini, mkoani Manyara.
Wananchi
wa Kijiji cha Ayamango, Babati Vijijini wakiwa na bango la asili lenye
maandishi yanayosisitiza umuhimu wa kuendelea na Muungano wa Serikali
mbili badala ya tatu.
Wazee wa Kijiji cha Ayamango wakimvisha mgolole,Kinana ikiwa ni heshima ya kuwa mmoja wa wazee wa kijiji hicho.
Wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii cha chama hicho wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Kinana
akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango, Babati
Vijijini. ambapo alikerwa kwa kiasi kikubwa na jinsi wananchi
wanavyoporwa maeneo yao na viongozi wa chama na Serikali ambapo aliahidi
suala hilo kulitafutia ufumbuzi kwa kulipeleka katika vikao vya juu vya
chama hicho.
Kinana akiwasikitishwa jinsi wananchi vijijini wanavyoporwa ardhi na kutumia mahakama kuchelewesha haki zao
.Kinana amesema kuwa viongozi wasiotimiza wajibu wao Mkoa wa Manyara atawaburuza kwa Rais.
Vijana wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za umoja wa vijana wa CCM kwenye mkutano huo
Wananchi wakiwa na bango linalosisitiza kendelea na mfumo wa Serikali mbili badala ya tatu
Kikundi cha vijana kikitumbuiza wakati wa msafara wa Kinana ulipowasili katika Kijiji cha Ayamango.
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment