Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na watanzania waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao
kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otani, wakati
akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo, Mei 21, 2014.
Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na watanzania waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao
kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otani, wakati
akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo, Mei 21, 2014.
Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
Baadhi
ya Watanzania waishio nchini Japan, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
alipokuwa wakiwahutubia katika hafla ya chakula cha jioni, iliyofanyika
kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, Mei 21, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na mwanamuziki Mtanzania wa bendi ya The Tanzanite, Abuu Omar,
wakati alipokuwa akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Japan,
waliohudhuria hafla hiyo ya chakula cha jioni. Kulia ni Mke wa Makamu,
Mama Asha Bilal.
Baadhi
ya Watanzania waishio nchini Japan, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
alipokuwa wakiwahutubia katika hafla ya chakula cha jioni, iliyofanyika
kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, Mei 21, 2014.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio nchini Japan, baada ya mazungumzo.
Baadhi ya Watanzania, waishio nchini Japan wakipiga picha ya kumbukumbu ya pamoja na ujumbe wa Makamu.
Na Mwandishi Maalum – Tokyo, Japan
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amewatoa wasiwasi Watanzania wanaoishi nchini Japan kuhusu mvutano
uliojitokeza ndani ya Bunge la Katiba na kuwahakikishia kuwa ana imani
Bunge hilo litakapokutana Agosti mwaka huu mambo yatakwenda vizuri .
Dkt.
Bilal amewatoa hofu Watanzania hao kufuatia risala yao iliyosomwa na
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo (Tanzanite Society) David Semiono kueleza
masikitiko yao kuhusu kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge la Katiba.
Akizungumza
na Watanzania hao katika ukumbi wa New Otani Hotel hapa Tokyo, Japan
jana Mei 21, 2014 Dkt. Bilal alisema kilichojitokeza katika bunge hilo
ni kurekebishana ili nchi iweze kupata Katiba mpya yenye maslahi kwa
wananchi na itakayodumu kwa miaka mingi ijayo.
Makamu
wa Rais alibainisha kuwa kazi ya kuandika katiba si rahisi kama wengi
wanavyofikiria kwani katika nchi zingine, wanafikia uamuzi huo baada ya
kutokea hali ya kutoelewana na hata kupigana jambo ambalo ni tofauti na
Tanzania ambapo uamuzi huo umefikiwa kiungwana kwa kuheshimu mawazo na
maoni ya wananchi wake.
“Sisi
kwa salama na amani tumeanza mchakato wa katiba mpya na tumalize kwa
salama na amani, tuendelee na sifa tuliyonayo ya umoja na mshikamano,”
aliasa Dkt. Bilal
Aliutaka
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuacha jazba na kurudi bungeni
ifikapo Agosti mwaka huu ili waweze kushirikiana na wenzao katika
kukamilisha kazi hiyo muhimu waliotumwa na wananchi.
“Tunachoomba
waliotoka nje ya mstari, tusiwe wa kwanza kukaidi na kufuata misingi ya
jazba. Tutangulize kwanza Utanzania wetu. Tunawaomba wote waliotoka
bungeni, warudi washirikiane na wenzao. Tukimaliza kwa amani mchakato
huu, tutakuwa tumeijengea sifa kubwa nchi yetu. Tumeheshimu matakwa ya
watu, sote tuheshimu mchakato huu mpaka tuufikishe mwisho kwa amani,”
alisema Makamu wa Rais.
Akizungumzia
Muungano, Makamu wa Rais aliwataka Watanzania hao kuendelea kuuenzi,
kuulinda na kuudumisha kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla, huku
akiwakumbusha kuwa muungano huu umekuwa wakupigiwa mfano Afrika na
duniani kwa ujumla.
“Muungano
wetu ni wakujivunia na wa aina yake barani Afrika na kote duniani.
Kumbukeni miaka ile nchi nyingi za Afrika zilijaribu kuungana lakini
zilishindwa. Safari ya miungano yao, ilikuwa fupi na miungano hiyo
imesambaratika,” alisema Dkt. Bilal huku akitolea mfano wa muungano wa
senego-Gambia na baadhi ya nchi nyingine za Kiafrika.
Akijibu
malalamiko ya Watanzania hao waliodai kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) haiwatendei haki wafanyabiashara wanaoingiza magari nchini kwa
kutoza kodi zenye utata bila hata kuzingatia taratibu zilizowekwa, Dkt.
Bilal alisema amelipokea tatizo hilo, na kufafanua kwamba Serikali
inaendelea kuzifanyia kazi kero mbalimbali ndani ya mamlaka hiyo.
Aliwataka
Watanzania hao kuwa na subra kwani alisema kila jambo huanza kwa hatua
moja na halimaliziki kwa siku moja na kuwahakikishia kwamba anaamini
kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kero hizo zitapatiwa
ufumbuzi haraka.Kuhusu ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya, Dkt.
Bilal aliiasa jamii na viongozi wa dini mbalimbali nchini kushirikiana
na serikali kwa kuwapa miongozo ya maadili mema vijana ili kuepukana na
janga hilo na hivyo Taifa liweze kupiga hatua ya maendeleo.
“Tusifanye
mzaha katika malezi ya watoto wetu, viongozi wa dini zote nchini wana
wajibu wa kuwafundisha vijana wetu maadili mema na sisi wazazi
tusichoke kuwakanya vijana wetu kwa ukali kuhusu matumizi ya dawa za
kulevya”, alisema Dkt. Bilal. Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo pia
kuhimiza Watanzania kutumia nafasi yao ughaibuni kushawishi wawekezaji
kuja kuwekeza nyumbani kwani Tanzania haiwezi kuendelea bila kuwa na
uwekezaji wa kutosha.
No comments:
Post a Comment