Baadhi
ya washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili ya mchujo katika
mashindano ya kusaka vipaji vya kuigiza yajulikanayo kama Tanzania Movie
Talents kwa kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha
Washiriki wa Tanzania Movie Talents wakipewa maelekezo
Baadhi
ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma muswada
(Script) mara baada ya kupewa kwaajili ya kuonyesha uwezo wao katika
kuufuata muswada
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions - Arusha
Shindano
la Tanzania Movie Talents limeendelea leo katika Ukumbi wa Triplle A,
Jijini Arusha ikiwa ni hatua ya pili sasa ya mashindano hayo kwa kanda
ya Kaskazini Mkoani Arusha.
Shindano
hili limeingia hatu aya pili mara baada ya kusitishwa hapo jana
Kutokana na Msiba uliotokea Wa Msanii na Muongozaji mahiri katika Tasnia
ya Filamu nchini, Marehemu Adam Philip Kuambiana aliyezikwa jana Katika
Makaburi ya Kinondoni na Kuhudhuriwa na Maelfu ya watu wakiwemo
viongozi wa Serikali na Wasanii wa tasnia mbalimbali nchini.
Shindano
la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho kwa washindi
watatu kutangazwa na majaji na hatimaye kila mshindi mmoja kuondoka na
kitita cha Shilingi laki tano taslimu na baadae washindi kuungana na
Washindi wa Mikoa Mingine kwaajili ya Fainali kubwa itakayofanyika
Katika jiji la Dar Es Salaam mwishoni mwa Mwezi wa Nane na mshindi
katika Fainali hiyo atajinyakulia Kitita cha Shilingi Milioni Hamsini za
Kitanzania (50,000,000/=).
Mpaka
sasa Mashindano ya Tanzania Movie Talents yashafanyika katika Kanda ya
ziwa Mkoani Mwanza, Kanda ya Kati Mkoani Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu
kusini Mkoani Mbeya , Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara na Sasa shindano
linaendelea Katika Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha huku Kanda ya Pwani
ikiwa ni kanda ya Mwisho katika Mashindano haya.
Tayari
Kipindi chetu cha Kwanza Cha Mwanza kimesharushwa katika Kituo Cha
Runinga cha ITV na vipindi vingine vitarushwa kila Jumamosi saa Nne
Usiku na kurudiwa Kila Siku ya Jumapili Saa Kumi Jioni na Jumatano Saa
Tano Usiku.
Shindano
la Tanzania Movie Talents linaendeshwa na Kampuni ya Proin Promotions
Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu
Tanzania.
No comments:
Post a Comment