Janneth Emmanuel (kushoto), Cresenciah Herman (katikati) na Joshua Wambura Stanslaus ambao ndio washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa wanaonyesha zawadi zao za pesa taslimu shilingi laki 5 kila mmoja mara baada ya kutangazwa washindi wa Kanda ya Ziwa.
Shindano la Kusaka VIpaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents limemalizika leo kanda ya ziwa, Mkoani Mwanza kwa washindi watatu kupatikana na kupewa zawadi zao. Washindi hao ni Janneth Emmanuel , Cresenciah Herman na Joshua Wambura Stanslaus huku binti mwenye umro mdogo kuliko washiriki wote Emiliana Fidelis mwenye umri wa Miaka 11 aliweza kung'ara kwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu tokea mwanzo hadi Mwisho wa mashindano haya na kuweza kuvuta hisia za majaji na kupelekea majaji kumtangaza mshindi wa shindano hili lakini kutokana na Umri wake kuwa ni chini ya kigezo cha umri uliohitajika hatoweza kwenda Dar Es Salaam Kwaajili ya fainali lakini majaji hawakumuacha bure walimpatia zawadi za Shilingi laki Moja kama ishara ya yeye kuwa Mshindi pia.
Baada ya Mashindano haya kumalizika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza sasa Zoezi linahamia Kanda ya Kati Mkoani Dodoma wiki hii ambapo Zoezi zima la usajili litafanyika kuanzi jumamosi ya tarehe 12 hadi 15 aprili ambapo pia watatafutwa washindi watatu pia wa kanda ya kati.
Washindi hawa watatu wataungana na washindi wengine watakaopatikana katika kanda zingine katika fainali itakauofanyika Mkoani Dar Es Salaam Na mshindi kupata Zawadi kubwa ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya 15 bora wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kuchaguliwa washiriki watano bora.
Hawa ndio washiriki walioingia tano bora
Emiliana Fidelis akiwa amesimama mbele ya meza ya majaji mara baada ya majaji kufurahishwa na kuvutiwa na Kipaji chake, Emiliana ni mmoja kati ya waliotakiwa kuwa mshindi wa Kanda ya ziwa ila kwa bahati mbaya Umri wake ndio ulikuwa kikwazo.
Jaji Yvonne Cherry akimkabidhi zawadi ya shilingi laki Moja Mshiriki Emiliana Fidelis mara baada ya kuvutiwa na Kipaji chake huku akiwa mshiriki pekee mwenye umri mdogo kuliko wote kwenye mashindano ya Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents.
Jaji Mkuu wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents, Roy Sarungi akimkabidhi zawadi mmoja wa Washindi watatu wa mashindano hayo mara baada ya kutangazwa washindi.
Jaji Single Mtambalike akimpongeza mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuibuka kidedea katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents.
Mshiriki Crensenciah Herman akilia kwa furaha mara baada ya Kutajwa kuwa mmoja kati ya washindi katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lilomalizika Leo Mkoani Mwanza
Majaji wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi watatu wa Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza mara baada ya Kuwatangaza na kuwakabidhi washindi zawadi zao.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza
No comments:
Post a Comment