Bwana Robert Foot akikabidhi funguo
za magari hayo kwa Kamanda wa mkoa wa Arusha ACP .Liberatus Sabas
Kamanda Sabas akitoa shukrani
zake kwa uongozi wa UN-ICTR kwa msaada huo. Katikati ni Afisa Habari wa
Mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inyoshughulikia
Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR) iliyo na makao yake makuu mjini Arusha imetoa msaada wa magari mawili ya kiusalama (Amoured Cars) kwa jeshi
la polisi mkoani Arusha ili kuimarisha shughuli zake za kiusalama mkoani
hapo.
Magari hayo ni baadhi ya yale yaliyokuwa yakitumika kwa shughuli za
usalama - kubebea watuhumiwa au watu nyeti - na mahakama hiyo inayotarajiwa
kumaliza shughuli zake mwakani. Magari hayo yameimarishwa kiusalama
ambapo hata risasi haziwezi kupenya kwenye bodi yake au kwenye kioo chake.
Magari hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala
wa Mahakama hiyo Bw. Robert Foot kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande
Liberatus Sabas.
No comments:
Post a Comment