Naibu
waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na
wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na
wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa
waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika
Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa
ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam
Mkurugenzi
Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor
akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa
kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa
kutoka Heifer International Tanzania umedhaminiwa na Mfuko wa Bill na
Melinda Foundation
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akifungua Pazia kuashiria Mradi huo wa
Kuendeleza sekta ya maziwa umezinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo jijini Dar Es Salaam.
Mjasiliamali
wa Maziwa kutoka Mkoani Iringa, Bi Diana akitoa Ushuhuda wake kwa
wageni waalikwa kuhusu mafanikio aliyoyapata akiwa kama mdau wa sekta ya
maziwa.
Mgeni
Rasmi katika Uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akimpongeza Mjasiliamali wa Waziwa
kutoka Mkoani Iringa, Bi Diana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuendeleza
Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na
wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini.
Baadhi
ya Wageni waalikwa na Wadau kutoka Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki
wakifuatilia mada kwa makini wakati wa UZinduzi wa Mradi wa Uendelezaji
Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Heifer International Tanzania na EADD pamoja na wadau wa
Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki.
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele ambae pia
alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Uendelezaji Sekta
ya Maziwa Afrika Mashariki akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya Kilolo
mara baada ya kumalizika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam
Mwishoni mwa Wiki.
No comments:
Post a Comment