PONGEZI NDANI YA RIADHA : GIDABUDAY AMPONGEZA FILBERT BAYI KWA KUTIMIZA MIAKA 40 TOKA AVUNJE REKODI YAKE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 2 February 2014

PONGEZI NDANI YA RIADHA : GIDABUDAY AMPONGEZA FILBERT BAYI KWA KUTIMIZA MIAKA 40 TOKA AVUNJE REKODI YAKE


Utaifa Kwanza Blog inatambua kazi nzuri iliyowahi kufanywa na mzee wetuFilbert Bayi. Hadi leo hii rekodi yake ni rekodi ya mashindano ya Jumuia ya Madola.

Magazeti mengi duniani yameripoti kumbukumbu hiyo nzuri kwake Filbert Bayi na kwa taifa letu la Tanzania kwa ujumla.
Nakumbuka maneno yake Bayi akisema“Myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni” Mzee Bayi anaheshimika sana ‘hata mimi namheshimu sana’ ila anastahili kuwa na ujasiri na uzalendo ule ule aliokua nao miaka 40 iliyopita katika uongozi wake ndani ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
‘Bila shaka anafurahi kufikia miaka 40 tangu avunje rekodi hiyo ambayo wengi aliokimbia nao huenda wameshatangulia mbele ya haki’ SASA MUNGU AKUPE NINI MZEE BAYI?
Tunamsihi mzee wetu aanze sasa ‘Mission’ nyingine ya kuweka rekodi tofauti; ambayo ni rekodi ya kuweka misingi mipya na imara ya kupata kizazi kitakachovunja rekodi kama yake.
Wilhelm Gidabuday, Mwanaharakati wa Michezo Tanzania.
Kufanya hivyo kutamweka Filbert Bayi katika ngazi nyingine kabisa ‘hapa duniani na mbinguni pia’ Mimi Gidabuday ninamtaarifu Filbert Bayikwamba ninampongeza sana kwa kutimiza miaka 40 tangu kufanya maajabu; ila BADO nitaendelea kumrekebisha pale atakapokosea njia, muda na wakakti wowote. HONGERA SANA KOCHA. Kwa maelezo zaidi Tembelea Blog Yake : www.gidabuday.blogspot.com

No comments:

Post a Comment