UKATILI WA KIJINSIA : MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUTOA PENZI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 9 February 2014

UKATILI WA KIJINSIA : MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUTOA PENZI



Jeneza la Marehemu, Sekunda Mushi (42), aliyeuwawa kinyama usiku wa kuamkia, Januari 6, wakiwa na majonzi katika mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kuuwa kwa sababu ya kimapenzi baada ya kuibuka kwa ugomvi kati yake na Mpenzi wake, aliyetajwa kwa jina la Gerald Mamkwe.

Jeneza la mwili wa Marehemu Sekunda Mushi likiingizwa kaburini katika maziko yaliyofanyika jana katika kijiji cha Longuo A, kata ya Uru Kusini, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Baba mzazi wa Sekunda Mushi (mwenye suti Nyuesi), akisikliza mahubiri ya mwisho katika ibada ya maziko ya mwanae, Sekunda Mushi, aliyeuwawa kikatili usiku wa kuamkia Januari 6 katika kile kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi.
Mzee Onesmo Mushi, ambaye ni Baba Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokana na ugomvi wa kimapenzi.
Mama Aurea Mushi, ambaye ni Mama Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokana na ugomvi wa kimapenzi.
Kwa Picha Ziadi Bofya hapa KIJIWE CHETU BLOG

No comments:

Post a Comment