MBUNIFU WA MAVAZI : ASIA IDAROUS AWASHUKURU WADAU WAKE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 19 February 2014

MBUNIFU WA MAVAZI : ASIA IDAROUS AWASHUKURU WADAU WAKE

Asia Idarous akipita kwenye red Carpet .wakati wa onyesho hilo.
Mbunge wa Bunge la Katiba, Mh. Maria Sarungi  akihojiwa na Deo wa Nivana wa East Afrika Television
Mmiliki wa Michuzi Media Group, Mr.Michuzi akishoo love na mkewe, siku hiyo
Asia akiwa na mumewe jukwaani, kushoto ni Miss Universe
Msanii Nemo akilitawala jukwaa siku hiyo.
Martin Kadinda miongoMAMA wa Mitindo nchini na Mkurugenzi wa Fabak Fashins, Asia Idarous Khamsin amewashukuru wadau mbali mbali kwa kuendelea kulinga mkono onyesho la Mitindo la kila mwaka la 'Lady in red' ambalo kwa mwaka huu limeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake huku likiwa la mafanikio kwa kuibua wanamitindo wakubwa hapa nchini.
Akizungumza Dar es salaam, katika ofisi za Fabak zilizopo Msasani jirani na Kwa Mwalimu Nyerere, Asia Idarous alishukuru wadau mbali mbali waliojitokeza siku hiyo sambamba na wadhamini waliofanikisha kwa shughuli hiyo kubwa hapa nchini.

Asia alisema ni jambo la fadhira  kwa kushukuru huku akiahidi kuboresha kama kulikuwa na mapungufu  ya hapa na pale. "Muungwana ni vitendo, ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ ilikuwa ni ya kipekee kwa mwaka huu, hivyo nawashukuru nyote kwa kuliunga mkono jukwaa la Lady in red 2014, kwa kutimiza miaka hii 10" alisema Asia Idarous.
Na kuongeza kuwa, kuelekea onyesho la mwakani kwa mwaka 2015, jukwaa hilo la Lady in Red, linatarajia kuwa la kimataifa ikiwemo wabunifu wa kimataifa kuonyesha ubunifu wao hapa nchini.
"Kwa sasa tunaelekea anga za kimataifa kupitia jukwaa hili hili la Lady in red, zaidi ni kuendelea kuliunga mkono ilikutimiza ndoto hizi,  na hii itasaidia kufungua milango ya wabunifu wetu kujiuza nje ya mipaka yetu" alisema Asia Idarous.
Onyesho hilo la Lady in red 2014,  lililotimiza miaka 10, lilifanyika  Februari 14, ndani ya ukumbi wa kisasa wa ndani ya hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Serena, ambapo siku hiyo pia ilikuwa ni maalumu kwa wapendanao duniani 'Valentine Day'  watu wa kada tofauti wakiwemo mastaa na watu maarufu walijumuika kwa pamoja kuliunga mkono onyesho hilo.
Wabunifu  mbali mbali wakiwemo magwiji na chipukizi walipata kuonyesha mitindo ya ubunifu kwenye jukwaa hilo  na kuvutia wengi siku hiyo. mbali na ubunifu wa mavazi, pia liliendana sambamba na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, huku asilimia kadhaa za mapato yake yalipelekwa kusaidia waathirika wa dawa za kulevya.
Kwa upande wa burudani, wapendanao na wadau waliojitokeza walishuhudia burudani  safi kutoka kwa wasanii mkali wa nyimbo za asili, Wanne Star na mkali wa R&B na Afro pop, Nemo ambaye  hadi sasa anatamba na vibao mbali mbali ikiwemo My Number One, alichomshirikisha Omy Dimpoz.
Pia Asia Idarous aliwashukuru wadhamini wakuu, ikiwemo kinywaji cha Zanzi na Rasta za Darling. Wengine ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ya jukwaa hilo ni pamoja na  Michuzi Blog, Vijimambo blog, Dj Bula, CXC, Times fm, Clouds media,  michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.
Mwisho
Habari na Andrew Chale,

(PICHA ZOTE KWA HISANI YA MICHUZI BLOG).

No comments:

Post a Comment