Vijana
wa Wakulima wakichoma matairi katikati ya barabara na kuzuia magari
kutopita eneo hilo kwa muda wa masaa sita, jambo lililosababisha foleni
kubwa ya magari na usumbufu kwa abiria, leo mchana. Askari wa kuzuia
ghasi walilazimika kutumia Risasi za moto na mabomu ya machozi ili
kuwatawanya watu hao na kuwafungulia njia abiria waliokuwa wamekwama
mahala hapo kwa zaidi ya masaa sita.
Askari
wakitoa tahadhari ya hatari kabla ya kuanza kuwatawanya vijana hao wa
wakulima, ambapo walilazimika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela,
Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa -
Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende
kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.
Wakulima
hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la
Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali sehemu za siri
na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika katika eneo hilo ambapo
wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha msongamano mkubwa
wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Morogoro, lakini wakulima
hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.
Baada
ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile, aliwaaamuru vijana wake kuwatawanya wakulima hao ambao
waligoma na kuanza kurusha mawe na askari hao wakajibu mapigo kwa kupiga
mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.
Katika tukio hilo jumla ya wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.
No comments:
Post a Comment