CLASS MATE'S SEND-OFF PARTY: MARY MEELA AMEREMETA KATIKA SHEREHE YA KUMUAGA ILIYOFANYIKA UHURU PEAKS GROUNDS ,JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 13 February 2014

CLASS MATE'S SEND-OFF PARTY: MARY MEELA AMEREMETA KATIKA SHEREHE YA KUMUAGA ILIYOFANYIKA UHURU PEAKS GROUNDS ,JIJINI ARUSHA

Bi. Mary Meela (kushoto) akiwa na uso mpana wa furaha katika sherehe ya kumuaga (Send off Party) na matron wake ambae pia ni class mate Bi. Tumaini Nnko iliyofanyika katika viwanja vya Uhuru Peaks Jijini Arusha.
Muda wa Shampeni ilihusika kwa wao wenyewe kufungua
Mawifi na Shemeji wakipata shmpeni...
Muda wa Keki ya Unga sasa......
Nilishe nikulishe kama ishara ya Upendo...
Keki moja kwa wakwe wa mzaa chema.....

Keki nyingine kwa Dada Mlezi wa Bi. Mary Meela mtoto kutoka hapo Moshi......
Ndafu hiyooo.....si unaelewa tena sisi watu wa Kilimakyaro bila huyu keki kazi haiendi kabisa chaa....

Ndafu kwa Wazazi wapenzi....
Kamti chukueni huyo ndafu mkamkatekate tule naniiiii.......
Shangazi anamtoa Bi. Mary Meela aelekee hukooo Musoma....



Zawadi toka kwa Mama.....ni ....BIBLIA TAKATIFU......Bila Mungu hakuna chochote hapa Duniani....
BIBILIA TAKATIFU HIYO HAPO SASA....

Wafanyakazi wenzake na Bi. Mary Meela kutoka DIAMOND TRUST BANK , tawi la Arusha nao wakimpongeza kwa kazi nzuri au maamuzi mazuri aliyoyachukua, ila yeye anafanya katika tawi la Mbeya .
Class mate Mwingine huyoooo Mary Kinisa a.k.a Posh (kushoto) akimpongeza Bi. Mary Meela kwa hatua aliyoifikia , ndoa sio mchezo .....!!!
Kapu la Mama sasa....!!!!

Anakabidhiwa kapu lenye vyombo mbali mbali....
WOSIA WA DADA.....dada yake na Bi. Mary Meela akimhusia kuwa CHUJIO hilo sio la kuchuja chai, bali la kuchuja mambo yote ya Umbea, Udaku, Ushakunaku, Ubazazi na uchafu wowote unaoletwa na watu , hiyo anapaswa kuchuja MANENO Hayo ili adumu kwenye Ndoa.
Piga maombi sasa ili Mume mtarajiwa afike sasa.....Baba katika jina la Yesu.....Huyu Jamaa atokee mwenyeewe bila mimi kumtafuta....
Yesu anajibu maombi ....amefika.....anamnyanyua kwa Upendo wa dhati...
Wanapendeza kweli kweli.......

Chakula sasa.......: Picha zote kwa hisani ya Class Mate wa nguvu Gadiola Emanuel The CEO wa Wazalendo 25 Blog / kwa maelezo zaidi piga hapa 0755 643 633 au 0715 643 633. KARIBU SANA.

No comments:

Post a Comment