MAZINGIRA MAGUMU: MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MJINI DODOMA ZIMESABABISHA HATARI KWA AFYA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 11 January 2014

MAZINGIRA MAGUMU: MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MJINI DODOMA ZIMESABABISHA HATARI KWA AFYA

Muuza Chipsi akiendelea kuandalia wateja wake huku maji machafu yakiwa  yametuama kibandani hapo hali inayotishia Afya za wateja wao, huku kilio cha wafanyabiashara hao kikielekezwa ofisi ya mhandisi wa manispaa kwa  wanaotoza kodi.

 Wateja wakiendelea kupata huduma ya chakula kwa mama lishe bila kujali  maji machafu yaliyotuama katika eneo hilo lililopo katika kituo cha  Daladala Jamatini Dodoma iliyisababisha na kukosekana kwa miundombinu.
 Maji yakiwa yamezagaa katika vibanda vya wafanya biashara wa chakula  (mama na baba lishe) kutokana na kukosekana na miundombinu ya kupitishi  maji pindi mvua zinaponyesha.

Na John Banda, Dodoma

WAFANYABIASHARA wa chakula (mama lishe) wamo hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza yakiwemo kipindupindu kutokana na maji ya mvua kutuama kwenye vibanda vyao ikiwemo kutengeneza harufu mbaya kutokana na kukaa kwa muda mrefu.

Mvua hizo zilizoanza kunyesha tangu mwishoni mwa mwezi uliopita zimekuwa zikisababisha kutuama kwa maji katika vibanda vya mama lishe wanaotoa huduma ya chakula katika kituo cha Daladala Jamatini Dodoma.

Wakiongea kwa niaba ya wenzao Martha Mboma, Zuhura Salumu na Doris Rebman walisema maji hayo yamewasababishia kuishi kwa hofu ya Afya zao kudhurika kutokana na uchafu unaosukumwa kutoka maeneo tofauti na kisha kuishia kwenye vibanda vyao.

Walisema hali hiyo imewasababishia kupoteza wateja ambao wanashindwa kwenda kupata huduma hiyo kutokana na kuhofia afya zao na wakati wao wamekuwa wakilipa manispaa kodi kila mwisho wa mwezi.

‘’Ona mwenyewe ndugu mwandishi kuna vinyesi vinaletwa na maji lakini pia watu wasio wastaarabu wamekuwa wakijisaidia haja ndogo kwenye chupa na kuzitupia kwenye maji hayo unadhani afya zetu zitakuwaje na hata hao wateja watakujaje au hawajipendi’’, alisema Mboma

Aidha alisema mvua hizo zilizoanza kunyesha tarehe Des 23, 2013 usiku zilijaza maji hayo na yakaa kwa muda mrefu kiasi cha kutengeza harufu kali iliyosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara japo wengine wameonekana hawaijali hali hiyo na kuendelea kutoa huduma bila

kutafuta ufumbuzi

Alisema tatizo hilo linatokana na ujenzi wa stendi hiyo mpya ambao haukuzingatia maji pindi mvua zitakapo nyesha ndiyo sababu ya walitengeneza bonde ambalo linaonekana kupokea maji toka pande zote wakati hakuna njia ya kuyatolea na wao kuruhusu mama lishe wapewe

maeneo katika eneo hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Haji Kulaya alisema tatizo hilo ni kubwa na tayali wameshawaona ofisi ya mhandisi wa manispaa zaidi ya mara nne kwa siku tofauti lakini wameshindwa kuchukua hatua yoyote zaidi ya kuishia kufika na kuangalia na kisha kutokomea.


Kwa upande wake Mhandisi wa Manispaa John Kitilla akiongea kwa njia ya simu alisema bado hajapata taarifa hiyo lakini atatuma watu kwenda kuona hali iliyopo na kisha watajua chakufanya baada ya kuona hali halisi iliyopo.

No comments:

Post a Comment