"SAY NO TO SEMBE ": MSICHANA WA KITANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 28 December 2013

"SAY NO TO SEMBE ": MSICHANA WA KITANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA.

 
 Msichana wa Tanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya akiwa amesimama karibu na meza yalipowekwa madawa yaliyotolewa kutoka kwenye mwili wake
Ni msichana gani wa Tanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini China? Hilo ni swali gumu ambalo kila mmoja amekuwa akijiuliza bila kupata jibu la uhakika. Mtandao wa chinadaily.com.cn umeandika habari na kuweka picha za kukamatwa kwa msichana huyo mwenye umbo refu, mwenye nywele ndefu na mweupe. Mtandao huo umeandika: Msichana mwenye miaka 28 kutoka Tanzania alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki madawa ya kulevya huko -Macao, Dec 19, 2013. Alikuwa ameficha kilo 1.1 za heroin zenye thamani ya $137,720 ( sawa na zaidi ya shilingi milioni 85) ndani ya mwili wake na kuchukua ndege kutoka Thailand hadi Macao. Alisema alikuwa akielekea Guangzhou, mji mkuu wa jimbo la Kusini mwa China Guangdong.

Madawa yaliyotolewa kwenye mwili wa msichana huyo mwenye miaka 28 yakioneshwa mbele ya waandishi wa habari
Tunafahamu kuna majina tayari yanayotajwa kuwa huenda wakawa ndio msichana huyo lakini hatuwezi kuyataja wala kuthibitisha kwa sasa ili kuepuka kuripoti habari zisizo na ukweli. 
 
 
Msichana wa Tanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya na aliyefunikwa uso wake akiwa chini ya ulinzi
Adhabu ya makosa ya biashara za madawa ya kulevya nchini China ni kifo.

No comments:

Post a Comment