Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Wizara na
Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jioni katika mkutano
maalum wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(kulia kwa Waziri Mwakyembe)na Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(kushoto kwa Waziri Mwakyembe
Katika ukumbi wa Karimjee,jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange akisisitiza
jambo wakati wa mkutano wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu
Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo. Mkutano huo umefanyika leo jioni katika
ukumbi Karimjee jijjini Dar es Salaam. Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo
amesisitiza ushirikiano na kujiwekea malengo katika utendaji kazi wa
kila siku.
Sehemu
ya Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na
wafanyakazi wa Wizara hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Dk. Shaaban Mwinjaka(Hayupo pichani) wakati wa mkutano
maalum wa kufunga mwaka na kuwatambulisha rasmi viongozi hao
uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tano kutoka kushoto), akiwa
katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Dk. Shaaban Mwinjaka (wa tano
kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica
Mwamunyange (wa nne kutoka kushoto) na Watendaji wakuu wa taasisi
zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi jana alipokutana nao ili
kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Uchukuzi na watumishi.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa kwanza kulia mstari
wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(wa
pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na wakuu wa Idara na Vitengo wa
Wizara ya Uchukuzi jana jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa
Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo
chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa WIzara hiyo.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk. Shaaban Mwinjaka(wa tatu kutoka kulia
mstario wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica
Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na baadhi ya
watumishi wa Wizara ya Uchukuzi jana jioni katika Mkutano maalum wa
Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa
taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment