Wachezaji wa Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao kwa
furaha baada ya kukabidhiwa kombe hilo kwa kuifunga Yanga katika mchezo
wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam. Katika mchezo huo Simba wameibuka washindi kwa.kuichapa Yanga
mabao 3-1, mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na Ramadhan
Singano huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.
Kiongozi wa Simba Hans Pope, akimpongeza Henry Joseph, baada ya mchezo huo.
Meneja wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi sh. 98
milioni Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa
kupata kura nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.Picha Zote na Muhidin Sufiani
No comments:
Post a Comment