Mtoto Kalebu Simwelu(6) enzi za uhai wake, mtoto huyu alichinjwa na kaka yake kwa madai kuwa baba yake alimrithisha mali zote. |
Mwili wa marehemu Kalebu ukiingizwa katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia. |
Ibada ya mazishi ikiendelea katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia |
Umati wa waombolezaji uliohudhuria maziko ya mtoto Kalebu ambaye aliuawa kwa kuchinjwa na kaka yake aliyedai kuwa baba yao amemuandikisha mali zote. |
Jamaa na ndugu wakiendelea na mazishi katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia ambako mtoto Kalebu alizikwa. |
KATIKA hali isiyo ya kawaida mmoja wa
watoto wa Diwani wa Kata ya Nkangamo Weston Simwelu(55) ambaye watoto wake
waliuawa kwa kuchinjwa na kunyongwa,Enock Simwelu(23) amekiri kufanya mauaji
hayo kwa madai kuwa yametokana na baba yao kumrithisha mali zote marehemu mdogo
wao.
Mauaji hayo yalitokea Disemba 19 eneo
la TAZARA katika mji mdogo wa Tunduma ambapo wauaji walivamia nyumbani kwa
Diwani huyo na kufanya mauaji ambapo walimchinja kwa kisu mtoto Kalebu
Simwelu(6) na mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge(17) na miili yao kuficha sebuleni
nyuma ya kochi.
Imeelezwa kuwa Enock pamoja na nduguye
wa mama mmoja Gabriel walishirikiana kwa pamoja kufanya mauaji hayo kwa madai
ya baba yao kufanya upendeleo kwa mdogo
wao Kalebu(6) ambaye ni mtoto wa mke mdogo wa baba yao.
‘’Chanzo cha mauaji hayo kimebainika,
mtoto wa mke mkubwa wa Diwani, Enock amekiri kuhusika na mauaji hayo
ameshirikiana na nduguye Gabriel Simwelu, madai yao, baba yao amemwandikisha
mali zote marehemu Kalebu, mtoto wa mke mdogo wa Diwani,’’amesema Kaimu Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la
Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda Masaki ni kwamba mmoja wa
watuhumiwa walioshikiliwa kwa ajili ya mahojiano ambaye ni kaka wa marehemu
aliyefahamika kwa jina la Enock Simwelu(23) amedai kukiri kufanya mauaji hayo
akishirikiana na mdogo wake aliyemtambulisha kwa jina la Gabriel Simwelu(19).
Kulingana na taarifa hiyo ni kwamba
mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye amehusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana
na tatizo la baba yake kuandikisha mali zote kwa mdogo wao ambaye ni mtoto wa
mke mdogo Kalebu Simwelu.
Kamanda Masaki alisema kuwa mauaji
hayo pia yalifanywa kwa kushirikiana na jirani na rafiki yao aliyefahamika kwa
jina la Patrick Msigwa(18) mkazi wa eneo la Majengo katika mji mdogo wa
Tunduma.
Mara baada ya kutokea kwa mauaji hayo
Jeshi la Polisi liliwanasa watu watano wakiwemo watoto wa mke mkubwa wa Diwani
Simwelu ambapo kulingana na madai ya awali ni kwamba chanzo kilitokana na
mgogoro wa kifamilia.
Wakati tukio hilo la mauaji linatokea
Baba wa marehemu Simwelu alikuwa shambani katika kijiji cha Kipaka ilhali mama
mzazi wa mtoto Tumaini Yohana(29) alikuwa kazini katika Ofisi ya Halmashauri ya
mji wa Tunduma.
Aidha mazishi ya mtoto Kalebu
yalifanyika Disemba 21 kwenye makaburi ya Nakonde katika mji mdogo uliopo
nchini Zambia na kuhudhuria na umati wa wakazi wa mpakani mwa Tanzania na
Zambia ambapo mwili wa mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge yalifanyika katika
kijiji cha Isansa wilayani Mbozi.(PICHA KWA HISANI YA SHOMI MTAKI-TUNDUMA)
No comments:
Post a Comment