Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, huko Maruhubi Mjini Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab, akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipotembelea jengo jipya la kiwanda cha uchapaji, Maruhubi jana,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiuliza suala kwa Mkurugenzi Kanda wa Kampuni ya MFI DOCUMENT SOLUTION LTD, Rama Subramanian,ikiwa ndio wataalam wa mshine za uchapishaji,alipotembela na kuona zinavyofanyakazi,wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda hicho,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,kuhusu mashine mpya zilizonunuliwa na idara ya uchapaji,wakati alipotembelea kuangalia mashine kuona utendaji wake kazi,baada ya kufanya unguzi rasmi,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa mashine ya CTP,ambayo inatoa picha kwa kutumia Plat,Mohamed Abass Rajab,(wa tatu kushoto) wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda cha Uchapaji cha Zanzibar jana,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
No comments:
Post a Comment