VIONGOZI WA CCM ZIARANI: KINANA, DR. ASHA ROSE MIGIRO NA NAPE WILAYANI RUNGWE, MKOANI MBEYA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 27 November 2013

VIONGOZI WA CCM ZIARANI: KINANA, DR. ASHA ROSE MIGIRO NA NAPE WILAYANI RUNGWE, MKOANI MBEYA




Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman Kinana akibeba tofali kushiriki ujenzi wa chumba cha, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, Nov 25, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe.


Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe.


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsaidia kupasua ubao fundi, John Mwandosya ( watatu), aliposhiriki ujenzi wa vyumbavya maabara katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Tukuyu. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo yenye umri wa zaidi ya miaka 60, Edward Mwantimwa.


Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipasua ubao, wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) aliposhiriki ujenzi wa  vyumba vya maabara, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, Nov 25, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alishiriki kupasua mbao kwa ajili ya ujenzi huo.


  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akisalimia wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kandete, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 25, 2013.


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akihutubia mamia ya wananchi katika Kijiji cha Kandete, wilayani, Rungwe, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani humo


Mamia ya wananchi wa Kata ya Kandete, wilayani Rungwe mkoani Mbeya wakimsikiliza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipohutubia mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata hiyo.


 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipewa zwadi ya kitenge kwa ajili ya mkewe, na kiongozi wa Kinana mama wa Kata ya Kindete,wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Salome Mwakalinga.


Mzee Issa Simon wa Kata ya Kandete, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, akimsimika Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwa Mzee wa Kinyakyusa, kabla ya mkutano wa hadhara uliofanywa na Kinana katika kata hiyo, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe. Baada ya kutawazwa alipewa jina la Mwakinana.


 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipewa zawa Salome Mwakalinga kwa niaba ya Kinana mama wa Kata ya Katende, Wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment