ZAIDI ya sh milioni kumi na mbili zimechangwa kwenye harambee katika Kijiji cha Samaria, wilayani Arumeru Mashariki, mkoani Arusha kwa ajili ya kuchangia uchimbaji wa visima vya maji.
Harambee hiyo iliongozwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari (CHADEMA) akiwa mgeni rasmi ambapo alifika kijijini hapo kushirikiana na wananchi.
Nasari alisema mbali na wananchi kuwa na changamoto hiyo, wanapaswa kuvumilia na kuonyesha ushirikiano wakati yeye akiendelea kufanya juhudi za kutatua kero hizo moja baada ya nyingine.
Hata hivyo aliwataka wananchi hao kuwafundisha watoto kuwa na tabia ya kuchangia michango mbalimbali ya kuleta maendeleo kama njia ya kuwajengea mazingira ya utoaji pale watakapokuwa watu wazima.
mbunge huyo aliwataka viongozi wa kisiasa kuacha masuala ya kisiasa na kuweka mbele masilahi ya wananchi katika kuleta maendeleo katika jamii.
Mmoja wa wananchi hao, Ndeshukurwa Andrea Mbise, alisema kero hiyo imesababisha baadhi yao kuoga mara moja kwa wiki, hata kutooga kabisa.
Kwa hisani ya:Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment