KILIMO KWANZA : TEKNOLOJIA YA KUHIFADHI ZAIDI YA LITA 6000 ZA MAJI NDANI YA SHAMBA LAKO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday, 14 November 2013

KILIMO KWANZA : TEKNOLOJIA YA KUHIFADHI ZAIDI YA LITA 6000 ZA MAJI NDANI YA SHAMBA LAKO

Teknolojia ya uhifadhi wa maji umeanzishwa katika vijiji mbali mbali katika wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha. jinsi ya kuandaa; unatakiwa uchimbe shimbo lenye futi 4 kwenda chini na upana wa futi 4 na urefu wa zaidi ya futi 6 itategemea na shamba lako lilivyo. Unaweka au kutandika karatasi chini ya shimo hilo na kubakiza karatasi la kufunikia, kisha unaweka aidha maji ya mfereji au unaweka ya bomba na pia unaruhusu maji ya mvua yaingie humo. Baada ya hapo funika  kwa matumizi yako binafsi ;kama vile ya kumwagilia mboga au kilimo cha umwagiliaji. Vijana changamkieni fursa hiyo ndani ya Kilimo Kwanza, wengi wamefaidika sana kupitia umwagiliaji na uhifadhi wa Teknolojia hii.
Maji yanavyoonekana yamejaa shimo na jinsi ya kufunika




No comments:

Post a Comment