TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI JUU YA AGIZO LA KAMATI YA BUNGE (PAC) KUHUSU VYAMA KUTOKUKAGULIWA NA CAG TANGU MWAKA 2009-2013. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 19 October 2013

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI JUU YA AGIZO LA KAMATI YA BUNGE (PAC) KUHUSU VYAMA KUTOKUKAGULIWA NA CAG TANGU MWAKA 2009-2013.



 
 
 

Kutokana na taarifa zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwa vyama vya siasa ambavyo vinapata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2009/2010- 2012/2013.

CHADEMA tunapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo juu ya taarifa hizo;

i. Kuwa taarifa hizo sio sahihi na hazina ukweli kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine, hii ni kutokana na ukweli kuwa tulishawasilisha taarifa zetu za fedha kwa msajili wa vyama vya siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/2011, 2011/2012 na hili linathibitishwa na barua ya msajili wa vyama vya siasa yenye Kumb.Na. CDA.112/123/01a/37, ya tarehe 04 september 2012. Iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa (nakala imeambatanishwa).

Aidha, hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010, tuliziwasilisha kwa Msajili wa vyama vya siasa kwa barua yenye Kumb.Na. C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya tarehe 27 Octoba, 2011. (Nakala ya barua imeambatanishwa).

ii. Kuhusu taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa mwaka huu wa fedha 2012/2013, bado haijawasilishwa kwenye ofisi za msajili wa vyama kutokana na barua ya msajili wa vyama vya siasa ya Novemba 26, 2012 yenye Kumb.Na.DA.112/123/16A/97 ambayo ilikuwa na maelekezo kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa, iliyokuwa inajibu barua tuliyomwandikia tukitaka kupata ufafanuzi kuhusu ukaguzi wa hesabu za chama kutakiwa kufanywa na CAG na alitujibu kuwa “tumefanya mawasiliano na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Serikali (CAG) kwa ufafanuzi wa jambo hili na tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika ukaguzi wa Mahesabu hayo”; mpaka leo hatujawahi kupata ufafanuzi huo pamoja na ukweli kuwa tumeshafunga hesabu zetu za mwaka kama chama (barua imeambatanishwa).
iii. Kuhusu taarifa ya fedha kutoka nje ya nchi, CHADEMA tumekuwa tukiwasilisha taarifa zetu kila mara tunapopata fedha kwa ajili ya mafunzo na programu nyingine mbalimbali za chama kama ambavyo msajili alituandikia barua tarehe 19 Agosti 2013 yenye Kumb. Na.DA.112/123/16a/10 iliyokuwa ni taarifa ya mapato yatokanayo na michango au misaada toka nje ya nchi, alisema “tunashukuru kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa” (imeambatanishwa barua husika).
iv. Kuhusu Taarifa za gharama za uchaguzi kwa mwaka 2010 , tuliwasilisha taarifa hiyo na Msajili alikiri kuwa ni vyama viwili tu ndiyo vilikidhi utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi kwa ukaguzi wa marejesho, hii inathibitishwa na barua ya Msajili yenye Kumb.Na. CDB.173/205/01/23 ya tarehe 16 April, 2012. (Nakala imeambatanishwa).

Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa CHADEMA ndiyo ambayo tulidai CAG awe na mamlaka ya kukagua fedha za vyama vya siasa ili taarifa zake ziwekwe hadharani na tutaendelea kutoa ushirikiano kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote, kuhakikisha sheria hii inatekelezwa ipasavyo kuhakikisha uwazi kwenye mapato na matumizi ya vyama vya siasa.

Aidha, kama ambavyo siku zote tumesimamia na kusisitiza, tunamtaka CAG akague fedha zote za vyama na sio ruzuku tu kama ambavyo kamati ya Bunge inataka iwe.

Imetolewa leo Alhamis, Oktoba 17, 2013;

……………………….
Antony C. Komu
Katibu wa Baraza la Wadhamini. 
 

No comments:

Post a Comment