MKUTANO WA SITA WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 9 October 2013

MKUTANO WA SITA WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa Mkutano wa Sita wa Vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendesha mkutano huo, leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaelekeza jambo, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati wa mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, leo kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
 8. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kikomunisti cha China CPC, Ai Ping, kwenye mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika. CPC kimealikwa kwenye mkutano huo kutokana na urafiki wake na CCM. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai).
 9. Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisaliana na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Frelimo cha Msumbiji Philipe Paunde wakati wa mkutano wa sita wa Makatibu Wakuu wa Vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika. leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha ZANU-PF, Didy Mutasa akionyesha alama ya hamasa ya chama chake, alipozungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano wa makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi mwa kusini mwa Afrika, kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana na Wanne kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 VIONGOZI wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, walioshiriki kwenye mkutano wa sita wa vyama hivyo, leo kwenye hoteli ua Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam, Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini, Gwede Mantash, Katibu Mkuu wa chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe, Didy Mutasa, Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chana Cha Kikomunisti cha China, Ai Ping,Katibu Mkuu wa MPLA cha Angola, Julio Paulo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama cha FRELIMO cha Msubiji, Philipe Paunde na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia,Nangolo Mbumba
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waandamizi, baada ya ufunguzi wa mkutano huo.Picha Zote na Bashir Nkromo

No comments:

Post a Comment