Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu
Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa
Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).Marehemu Nyaisangah
atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na
vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya
Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akiwasili kwenye Viwanja vya
Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo kushiriki Kuaga Mwili wa Marehemu
Julius Nyaisangah.Wanaompokea ni Wajumbe wa Kamati ya Mazishi (kushoto)
ni Aboubakar Liongo na kulia ni Teddy Mapunda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi
wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam
kuungana na Waombolezaji wengine kuaga Mwili wa Marehemu Julius
Nyaisangah. Kwa Picha Zaidi >>> BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment