GIDABUDAY ASEMA "TOC / RT HAPATOSHI: HARAKATI ZA WADAU ZAKWAMISHA UWIZI ULIOZOELEKA; IAAF YAKATAA KUTOA $200,000 (TSHS: 330,000,000)" - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 28 October 2013

GIDABUDAY ASEMA "TOC / RT HAPATOSHI: HARAKATI ZA WADAU ZAKWAMISHA UWIZI ULIOZOELEKA; IAAF YAKATAA KUTOA $200,000 (TSHS: 330,000,000)"

Filbert Bayi/Katibu wa TOC
Tanzania kuna chombo maalum kiitwacho TAKUKURU kazi yake ni kuzuia na kupambana na rushwa; lakini taasisi fisadi kuliko zote Tanzania (TOC) haijali jina la chombo hicho cha kuzuia na kupambana na rushwa. 
Vugu vugu za harakati zilizoanza 2012 kabla ya mashindano ya Olimpiki ya London imeanza  kuzaa matunda baada ya Chama Cha Riadha Cha Dunia (IAAF) kukataa kutoa fedha hizo zilizokuwa zikitolewa kila mwaka na IAAF, ambapo kigezo kikubwa kilikuwa matumizi mabovu.

Fedha hizo ambazo huwa zinaidhinishwa na sahihi za viongozi wa RT na kuishia mfukoni mwa bosi wa TOC, safari hii imegonga mwamba baada ya nyaraka hizo kuchunguzwa kwa makini na kugundulika kwamba zina kasoro nyingi na zinaashiria ufisadi mtupu. 

Watanzania tujiulize fedha hizo huwa zinaliwa na mchwa gani? ni matumaini yangu sasa watanzania wataendelea kufunguka macho na masikio na kufahamu kwamba huo mchezo mchafu husababisha TOC kusimamia kidete KATIBA na CHAGUZI za RT ili VIBARAKA wa kusainishwa kirahisi wachaguliwe wao (TOC) waendelee kutafuna mbavu za taifa letu.

Bila aibu “wanataka kuunda kamati ya kukimbiza fimbo ya Malkia kwa kumshirikisha raisi wa Tanzania”, Bila shaka mbinu hizo za kimafya za kumshirikisha rais wa Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na swahiba wa TOC Leonard Thadeo.

Harakati zitaendelea maana harakati zina nguvu kushinda TAKUKURU! "Utaifa Kwanza" . Source: www.gidabuday.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment