KATIBU MKUU WA CCM AKIENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI SIMIYU NA MEATU - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 16 September 2013

KATIBU MKUU WA CCM AKIENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI SIMIYU NA MEATU


5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kata ya Ngoboko, huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio hilo.7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa CCM kata ya Ngoboko mara baada ya kushiriki shughuli za ujenzi wa jengo hilo.
 11Hili ni Daraja la mto Mwanhuzi mjini Meatu ambalo limejengwa na serikali na linatarajiwa kuzinduliwa siku chache zijazo baada ya kukamilika,Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pia alikagua daraja hilo katika moja ya shughuli alizofanya katika ziara hiyo kama wanavyoonekana mafundi wakiendelea na kazi ndogo ndogo zilizobaki.  
8Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM ndugu Nape Nnauye katikati Mh. Luhaga Mpina Mbunge wa Jimbo la Kisesa na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Ndugu Dk Titus Kamani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman wakati alipokuwa akizungumza na wanaCCM wa Kata ya Ngoboko. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- MEATU SIMIYU).

No comments:

Post a Comment