CHEKI FIESTA 2013 NDANI YA MJI WA SINGIDA ....NOMAAAA SAAAANA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 26 August 2013

CHEKI FIESTA 2013 NDANI YA MJI WA SINGIDA ....NOMAAAA SAAAANA

Pichani kulia ni Niki wa Pili na shoto ni kaka yake Joe Makini,wote ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a hip hop wakiwa sambamba na mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu wakishangilia jambo nyumba ya jukwaa.
Msanii Muigizaji wa filamu na muziki wa bongofleva,Shilole pichani shoto akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,ndani ya Singida Motel.
 Sehemu ya umati wa watu wakishangilia burudani iliyokuwa ikiendelea kwenye kiota hicho cha Singida Motel.
 Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature akiwa na wasanii wenzake wa kundi la TMK -Wanaume Halisi,wakilishambulia jukwaa vilivyo.
 Mashabiki waliokuwa wamejibanza ubavuni mwa jukwaa,nao walikuwa wakipata ile kitu roho inapenda kutoka kwa wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
 Chumaaaa a.k.a Chid Benz akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
 Anajiita mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiimba nyimbo zake za mahaba,mbele ya maelfu ya wakazi wa singida na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
 Ommy Dimpo a.k.a pozi kwa pozi akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani
Kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa
 Dj Mahiri kutoka Clouds FM,Dj Zero akifinya finya mashine zake kwa namna ya pekee kabisa,iliyokuwa ikiwafanya mashabiki kibao wazidi kuchenguka na kupiga mayowe kila wakati.
 Wenywewe wanajiita Makomando,wakilishambulia jukwaani kwa pamoja usiku huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea ndani ya Singida Motel.
Ni full kujiachia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,wengine wakiwa juu ya miti aaahhh nomaa sanaaa.!
 Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Singida wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linalofanyika kwenye viwanja vya Singida Motel usiku huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Petter Msechu akiwaimbisha mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 linaloendelea hivi sasa ndani ya Singida Motel.
 Ni ndani ya Singida Motel tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea hivi sasa 
 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Lina na Amin wakilishambulia jukwaa kwa pamoja,huku wakazi wa Singida waaliofurika usiku huu ndani ya Singida Motel wakipiga mayowe ya shangwe.
 Amin Jukwaani akiwambisha mashabiki wake,huku mayowe kila kona yakisikika usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida. Kwa picha zaidi bofya hapa >>>

No comments:

Post a Comment